-->

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DK. HUSSEIN MWINYI ASISITIZA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUJIANDAA NA TATIZO LA UGAIDI NA UHARAMIA

Friday, September 16, 2011

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi


Na Salama Njani, Habari Maelezo zanzibar

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi amesema kuwa nchi za Afrika Mashariki lazima zijiweke tayari katika kukabiliana na tatizo la ugaidi na vitendo vya uharamia.

Waziri huyo alieleza hayo leo huko katika kambi ya kijeshi Chukwani nje kidogo ya mji alipokuwa akifungua mafunzo ya ‘Natural Fire 11’, yanayowashirikisha wanajeshi kutoka nchi za Afrika Mashariki na Marekani.

Alisema nchi za Afrika Mashariki lazima zijiweke tayari katika kukabilina na ugaidi na uharamia ambao bado unaonekana tishio katika ukanda huo.

Alisema matatizo hayo kimsingi yanatokana na kutoepo kwa serikali dhaifu nchini Somalia, inayoshindwa kudhibiti vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikisambaa ndani ya nchi za Afrika Mashariki.

“Vitendo hivi vimeshamiri nchini Somalia, hivi sasa vimekuwa vikipenyeza kwa kasi na kuenea katika nchi za Afrika Mashari, mafunzo haya yatavisaidia vikosi vyetu kutambua mbinu za kisasa na kujiweka tayari kukabiliana navyo”, alisema waziri huyo.

Alisema mbali ya mafunzo hayo kulenga katika kujifunza mbinu za kukabiliana na ugaidi na uharamia, pia yatawasaidia wanajeshi hao kutambua mbinu za ulinzi wa amani pamoja na namna ya kukabiliana na maafa.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunjange alisema jeshi ndio nguzo ya amani ya nchi, hivyo lazima maofisa na wapiganaji wawe na mbinu zitakazo saidia kukabiliana na vitisho hasa vya ugaidi na uharamia.

Alisema mazoezi hayo yamekuja katika wakati muafaka ambapo vikosi vya nchi hizo vitazidisha mashirikiano baina yao.

Kwa upande wake Bregedia Jenerali James Owens kutoka jeshi la Marekani, alisema jeshi la Marekani linajivunia kuwa na uhusiano na urafiki na majeshi ya nchi mbali mbali za Afrika.

Alisema hatua hiyo itarahisisha kukabiliana na matizo ya vitisho vya kiusalama kila pale yatakapojitokeza.
“Tunachotaka kukiona kikiendelea ni urafiki na uhusiano wa karibu baina yetu na vikosi vya nchi mbali mbali kutoka Barani Afrika”, alisema Owens.

Naye Enos Bukuku akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki, alisema kanda ya Afrika Mashariki itaweza kupiga hatua za kimaendeleo katika uchumi endapo eneo hilo litakuwa kwenye hali nzuri ya kiusalama.

Alifahamisha kuwa vikosi vya ulinzi vina wajibu wa msingi wa kuhakikisha nchi za Afrika Mashariki zinakuwa salama katika kuepukana na vitisho vya ugaidi na uharamamia.

Mafunzo ya ‘Natural Fire 11’ ambayo yanafanyika katika kambi ya jeshi Chukwani yamefunguliwa leo na yanatarajia kufungwa tarehe 20 mwezi huu.


No comments:

Newer Post Older Post

UNAPOHITAJI kujua DUNIANI nini kimetokea, Basi fuatilia Kurasa Zangu za Kijamii TWITTER, FACEBOOK pamoja na INSTAGRAM, BONYEZA hapa >>> TWITTER, INSTAGRAM na FACEBOOK, PIA Unaweza Kujiunga na chaneli yangu ya YOUTUBE, ili kutazama Video >>>YOUTUBE

 

Copyright © 2010 NYUMBANI KWANZA. All Rights Reserved.