-->

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Sunday, July 31, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 31, 2011


STARS v, CHAD KOMBE LA DUNIA 2014


Upangaji makundi ya mechi za mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil ulifanywa jana (Julai 30 mwaka huu) karibu na ufukwe wa Copacabana jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Jerome Valcke.


Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco na Gambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimika kucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad.


Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15 mwaka huu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiye atakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwenda Brazil.


Stars ni miongoni mwa timu 29 ambazo kwenye viwango vya ubora vya FIFA vya Julai mwaka huu katika Afrika ziko chini ya timu 24 bora, hivyo kulazimika kuanzia hatua hiyo ya kuchujana zenyewe kabla ya kuingia hatua ya makundi ambayo itachezwa kuanzia Juni 1, 2012 hadi Septemba 10, 2013.


Kwa mujibu wa viwango vya FIFA vya Julai mwaka huu, Tanzania iko katika nafasi ya 127 wakati Chad ni namba 158. Kwa upande wa Afrika, Tanzania ni namba 33 na Chad 43. Nchi 52 kati ya 53 za Afrika zimeingia katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Ni Mauritania pekee ambayo haikuthibitisha ushiriki wake.


Timu 10 za juu kwa ubora barani Afrika ambazo zimeongoza makundi 10 ya Afrika katika upangaji ratiba ni Afrika Kusini, Tunisia, Cote d’Ivoire, Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Misri, Algeria, Cameroon na Senegal.


Afrika ina nafasi tano kwenye fainali za Kombe la Dunia, huku Ulaya ikiongoza kwa kuwa nazo 13.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
» » »

HAINA MAJOTROOOOOOOO, YABAMBA LEADERS CLUB KATIKA MSIMU WA DHAHABU UNAOENDELEA KATIKA SERENGETI FIESTA 2011

"Twenzetu Mamaa Tukamuone LUDACRISS"

Hapa tuko Njiani tukiingia katika Viwanja Vya LEADERSMuslim, Hussein na Dr. BHussein, akiwa na Speciroce pamoja na ndugu zake


Victa naye hakukosa tulikutana Naye ndani ya LEADERS

haa haaa haaaaaaainaaaaaa Majotrooooooooo

Umati uliofurika katika Viunga vya LEADERS katika Serengeti FIESTA 2011Ludacris


Kwa habari za PICHA zaidi :-


tembelea HAPA, HAPA, HAPA, HAPA, HAPA na HAPA

» » »

JILIWAZE NA ACUDO IMPACT: VIDEO

Thursday, July 28, 2011

» » »

YALE YALE TENA BUNGENI

WENJE ATOLEWA KWA NGUVU, MBUNGE CCM ANUSRIKA KUPIGWA

MBUNGE wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, jana alijikuta akitolewa bungeni na askari (wapambe) wa Bunge waliotii amri ya Mwenyeviti wa Bunge, Sylivester Mabumba, aliyeongoza kikao siku hiyo.Katika tukio ambalo ni la kwanza kutokea tangu kuanza kwa Bunge la Kumi linaloongozwa na Spika Anne Makinda, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alinusurika kupigwa na wabunge wa kambi ya upinzani baada ya kuwakejeli Chadena akisema waache mambo ya kitoto.

Mabumba alitoa amri ya Wenje kutolewa nje baada kukaidi amri ya Mabumba kumtaka akae chini mbunge huyo wa Nyamagana alipokuwa akiomba mwongozo, katikati ya mabishano yaliyokuwa yakiwajumuisha wabunge wengine wakati huo.Wakati Wenje akisisitiza kuomba mwongozo kwa maelezo kwamba jambo analotaka kusema "lina maslahi ya nchi", Mabumba ghafla aliwaita askari (wapambe) wa Bunge na kuwaamuru wamtoe nje kwa kukiuka kanuni za Bunge.

Kabla ya kuwaita askari hao, Mabumba ambaye ni Mbunge wa Dole alikuwa amemwamuru mara tatu Wenje akae chini, lakini hakutii akisema: "Nina jambo la dharura ambalo ni kwa maslahi ya Taifa".

"Sargent Ant Arms, mtoe nje mheshimiwa Wenje," alisema Mabumba na hapo askari watatu waliingia na kumtoa nje Wenje, tukio ambalo liliacha kukiwa hakuna utulivu bungeni.

Pamoja na kusindikizwa na askari wa Bunge, baadhi ya wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi walitoka nje wakimsindikiza Wenje.Walipofika nje ya ukumbi wa Bunge walianza kumlalamika kwamba, Mabumba ameshindwa kuongoza Bunge na kudai kuwa anaonyesha upendeleo wa wazi katika uendeshaji wa vikao vya chombo hicho.

Nje ya Ukumbi wa Bunge
Nje ya Ukumbi wa Bunge ilizuka tafrani nyingine iliyosababisha Mbunge Filikunjombe (CCM), kunusurika kupokea kichapo kutoka kwa wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi baada ya kuingilia mazungumzo yao wakati wanajadili suala la Wenje kutimuliwa ukumbini.

“Tatizo lenu ninyi wabunge wa Chadema mnaishia kuwa wabishi kila wakati, jambo ambalo linawapotezea heshima kwa wananchi,’’ alisema Filikunjombe na kuongeza: “Acheni mambo ya kitoto rudini ndani kuendelea na Bunge. Sio kila siku ninyi Chadema tu, watu wamewachoka.’’

Kauli ya ilikuwa kama kumwaga petroli kwenye moto, kwani kundi la wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi ambao kwa wakati huo wakiongozwa na Moses Machali (Kasulu Mjini NCCR), walimvaa kama nyuki mbunge huyo na kuanza kurushiana maneno makali.

“We mjinga kweli, hapa sio wabunge wa Chadema hata sisi wa NCCR-Mageuzi tupo tunachojadili ni maslahi ya nchi sio ushabiki wa vyama, toka hapa mshamba wewe,’’ alisema Machali.

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Susan Kiwanga, alimwambia Filikunjombe aache hadithi za kijinga kwani wananchi wa eneo lake wanaporwa chuma, lakini yeye (Filikunjombe) anashindwa kuwatetea badala yake anarukia mambo yasiyomuhusu.“Tuondolee ujinga wako hapa, wananchi wako katika maeneo ya Liganga wanaporwa mali usiku na mchana unashindwa kuwatetea leo unapotuambia tuna akili ya kitoto, hivi unataka Watanzania wafe ili ninyi mshangailie,’’alisema Kiwanga.

Wabunge wengine waliomwandama zaidi Mbunge huyo ni, Machali (NCCR-Mageuzi), Peter Msigwa (Iringa Mjini-Chadema), Mariam Msabaha na Susan Kiwanga wote wa Viti Maalum (Chadema) ambao walimzingira mbunge huyo na kuanza kumrushia maneno ya kejeli.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya wabunge wengine wa Chadema, Godbles Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Vicent Nyerere (Musoma Mjini) walipoingilia ugomvi huo na kutaka Filikunjombe awaombe radhi, lakini alikataa.Kama si busara iliyotumiwa na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM) hali ingekuwa mbaya kwani idadi ya wabunge wa Chadema ilipozidi yalisika maneno kuwa mbunge huyo apigwe, ndipo Nkamia alipofika na kuokoa jahazi akimtaka Filikunjombe aondoke katika eneo hilo.

Maelezo ya Wenje
Wenje aliwaambia waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge kuwa kitu alichokifanya hakikustahili adhabu kama aliyopewa kwa kuwa alikuwa sahihi. '' Pale mimi nilikuwa sahihi kabisa kwani sikutaka kuzungumzia suala la Lissu bali nilikuwa nazungumzia suala la masilahi ya Watanzania wote. Ikumbukwe kuwa kuna samaki walioingizwa bila polisi kujua na sasa wako sokoni wananchi wanakula hiyo ni hatari, sasa mwenyekiti anasema kuwa nitoke hajui kanuni yule,'' alisema Wenje.

Mbunge huyo alisema kitendo cha Mwenyekiti kuamuru atolewe nje kwa amri ni kukiuka kanuni na kwamba hajui kwani aliposema suala la dharula ni pale kunapotokea vita si kweli. '' Kanuni ya 47 (1-3) ndiyo niliyotumia na inaniruhusu kabisa kuomba mwongozo huo, kwani wananchi wanaumia halafu tunaambiwa hadi kuwe na vita, kama si umbumbumbu ni nini basi," alihoji Wenje akiwa ameshika kitabu cha Kanuni za Bunge.Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chedema) alisema kinachomsumbua Mwenyekiti ni kutokujua kanuni.

Chanzo cha mtafaruku
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ndiye aliyeanzisha balaa ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kueleza kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa amesema uwongo bungeni.

Lissu alisema Majaliwa alipokuwa akijibu swali lake namba 313 kuhusu michango kwa wananchi, amedanganya kuwa wananchi hawalazimishwi kutoa michango hiyo na kusisitiza kuwa ana ushahidi unaothibitisha kwamba michango hiyo ni lazima.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haitumii nguvu katika kuwatoza wananchi michango hiyo, bali wanashirikishwa katika kuibua, kupanga na kuendesha miradi yao wenyewe,’’ alisema Naibu Waziri Majaliwa.Baada ya majibu hayo, Lissu alisimama na kulieleza Bunge kuwa Naibu Waziri alisema uongo huku akinukuu barua ya Mkuu wa Wilaya ya Singida iliyotolewa Mei 2,2005.

habari kwa Hisani ya gazeti MWANANCHI, soma zaidi HAPA
» » »

WAJIBU WA WAANDISHI KATIKA JAMII

VYOMBO vya habari vinawajibu wa kuwaunganisha wananchi Zanzibar, umuhimu wa kuwa na serikali ya Umoja wa Kitaifa, hasa baada ya wananchi hao kupita katika kipindi kigumu na cha muda mrefu cha hitilafu za maelewano zilizotokana na hali ya siasa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alieleza hayo jana lipokuwa akitoa mada kwenye warsha ya siku mbili inayoelezea nafasi ya vyombo vya habari katika kuimarisha serikali ya Umoja wa kitaifa.

Mhadhiri huyo alisema kihistoa Zanzibar imepitia katika mkondo mrefu wa kihistoria wa kuhitilafiana kisiasa hali ambayo imezikwa na maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa baina ya vyama vya CUF na CCM.

Alifahamisha kuwa baada ya kupatikana kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo imekuwa msingi imara wa utengamano baina ya Wazanzibari hivi sasa umefika wakati wa kuzienzi na kuzitunza tunu za taifa.

Alizitaja tunu hizo ambazo haziwawekwa katika utaratibu mzuri na aadhi yao zinahitaji kufanyiwa mapotio ni pamoja na amani, umoja,, uzalendo, mashikamano, usawa, haki, muungano, uvumilivu katika dini, rangi na siasa.

Muwezeshaji huyo alisema jamii ipaswa kuelimishwa kwa undani umuhimu wa tunu hizo ambazo zina umuhimu mkubwa katika kujiletea maendeleo, na kueleza kuwa kazi hiyo inaweza kufanywa kwa usahihi na vyombo vya habari.

Kwa upande wake Rashid Omar Kombo ambaye ni Muhadhiri wa Chuo cha Habari Zanzibar, akiwasilisha mada katika warsha hiyo alisema vyombo vya habari vinawajibu wa kuitathmini hali ya utawala bora kwa kutumia viashria vilivyopo hasa wakati huu ambapo Zanzibar ina serikali ya umoja wa Kitaifa.

Alisema utawala bora unamchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya nchi yoyote sambamba na upatikanaji wa haki za msingi ambazo kila mwanadamu anatarajiwa kuzipata bila ya kuwepo mizengwe yeyote.

Wakichangia washiriki wa warsha hiyo walipendekeza uwepo uwajibikaji wa vyombo vya habari katika kutoa taarifa sahihi kwa wasikilizaji, wasomaji na watazamaji wa vyombo vyao na kutaka uweledi utumike ili kuepusha kuandika habari zinazoweza kusababisha mifarakano katika jamii.

Awali akifungua warsha hiyo waziri wa Bishara na Viwanda, Nassor Ahmed Mazrui, kwa niaba ya waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na Michezo, Abdillahi jihad Hassan, alivitaka vyombo vya habari viandike habari zao kwa misingi ya uweledi ili kuepuka kuwa msingi wa mitafaruku katika jamii.

Waziri huyo alisema umefika wakati wananchi kuelimishwa na kuzielewa tunu za taifa ikiwemo Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964, ambayo ndiyo yaliyomkomboa kila Mzanzibari.

soama zaidi HAPA
» » »

JENERETA NI MZIGO KWA ZECO

Wednesday, July 27, 2011

Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Gulioni ambapo pamoja na mambo mengine alikanusha maneno ya baadhi ya wawakilishi kwamba majenereta yalionunuliwa na shirika lake kuwa mabovu

SHIRIKA la Umeme Zanzibar (ZECO), limesema genereta za umeme wa dharurazilizonunuliwa na serikali hazifanyikazi kutokana na gharama kubwa za uendeshajina sio kuharibika.
Meneja Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Ali Mbarouk alieleza hayo jana alipokuwaakizungumza na waandishi wa habari ofisini wake Gulioni mjini Zanzibar.


Alisema tofauti na inavyodaiwa, ukweli ni kwamba genereta hizo zimeshindwakufanyakazi ya kuzalisha umeme kutokana na gharama za uendeshaji ambapo kwa sikuhutumia lita 8,000 kwa siku.


Alisema shirika hilo limesitiza kuzitumia katika kuzalishia umeme kwanizinahitaji gharama kubwa ambapo kuanzi mwezi Agosti mwaka jana hadi Machi mwakahuu jenereta hizo zimetumia kiasi cha sjilingi milioni 900.


“Ukweli ni kwamba genereta zetu zote nzima hakuna mbovu hata moja, ila tatizo nigharama za uzalishaji”, alisema Meneha huyo.


Alifahamisha kuwa uzalishaji wa umeme unagharama ya shilingi 394 kwa uniti mojaikilinganishwa na bei ya shilingi 120 wanayouziliwa wateja wa Zanzibar.


Jenereta hizo 32 zilinuliwa na ili kuupunguzia mzigo waya wa umeme unaotokaTanzania bara ambao umechaa na hauna uwezo wa kuchukua zaidi ya megawati 40,huku matumizi kwa kisiwa cha Unguja kikikiwa kinatumia zaidi ya megawati 55.


Akizungumzia deni la TANESCO ambapo hivi karibuni walikaririwa wakisema kuwawanalidai shirika hilo bilioni 50, Meneja huyo alisema shirika lakehalikubaliani na deni hilo kwani kuna utata mkubwa uliojitokeza.


“Tanesco wanatudai lakini sio deni bilioni 50, hili ni denilililoengezwa”,alisema Meneja huyo.
Meneja huyo alilishutumu EWURA kwa kuongeza bei ya umeme Zanzibar ambapo watejawamepandishiwa kwa zaidi ya asilimia 168 jambo ambalo alisema sio sahihi nalinawaumiza sana wananchi.
» » »

NGOMA AFRICA BAND KUTINGISHA MAGHOROFA FRANKFURT CITY,JUMAMOSI 6.08.2011

Tuesday, July 26, 2011

FFU wa Ngoma Africa band Jino kwa Jino na washabiki wa
Africa & Carebbean Festival, Frankfurt ,jumamosi 6.08.2011
"Bongo Tambarare" bado inapasua anga mtandaoni !
Maelefu ya washabiki mjini Frankfurt wanatarajiwa kuvaana uso kwa uso,
jino kwa jino na bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya
"Ngoma Africa band" katika onyesho kubwa la kimataifa la "Africa &
Carebbean Festival,litakalo fanyika katika viwanja vya Robestock Park,
mjini Frankfurt,Ujerumani siku ya jumamosi 6.08.2011,ambako kamanda Ras Makunja
wa FFU ataongoza kikosi chake jukwaani,bendi hiyo yenye utajili wa washabiki na wanamziki
wenye vipaji miongoni mwao akiwemo mpiga solo gitaa Chris-B.

Ngoma Africa band wanatamba na nyimbo yao mpya ambayo ni zawadi ya miaka 50 uhuru,
nyimbo hiyo "Bongo Tambarare" inasikika katika kambi ya FFU at

www.ngoma-africa.com
» » »

VIINGILIO U23 v SHELISHELI

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (U23) itacheza mechi mbili
za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu ya Taifa ya Shelisheli kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha. Kiingilio cha chini katika
mechi hizo kitakuwa sh. 3,000.


Kwa jukwaa kuu kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kiingilio kingine ni sh.
5,000. Timu ya Shelisheli tayari iko jijini Arusha ambapo iliwasili Julai 22
mwaka huu mchana ikitokea Nairobi, Kenya tayari kwa mechi hizo.
Mechi ya kwanza itachezwa Julai 27 mwaka huu, wakati nyingine itakuwa Julai 29
mwaka huu. Mechi zitaanza saa 10 jioni, na Shelisheli inatarajia kuondoka nchini
kurejea kwao Julai 30 mwaka huu kwa kupitia Nairobi.


U23 ambayo iko chini ya kocha Jamhuri Kihwelo imeondoka leo asubuhi (Julai 25
mwaka huu) kwenda Arusha. Itafanya mazoezi yake ya kwanza jijini humo leo jioni
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta.


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen pia yuko na timu hiyo akitoa ushauri wa
kiufundi baada ya kuongeza wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’ wa Simba, Juma Seif
Kijiko wa Yanga na mfungaji bora wa michuano ya Kili Taifa Cup, Gaudence
Mwaikimba wa Moro United kwa lengo la kuangalia viwango vyao kwenye mechi hizo
ili kuona kama watamfaa kwenye kikosi cha Stars.


Baada ya mechi hizo, Julai 30 mwaka huu jijini Arusha, Poulsen atataja kikosi
cha Stars ambacho kitaingia kambini Agosti 2 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya
kirafiki ya kimataifa dhidi ya Palestina.


Taifa Stars inatarajia kuondoka Agosti 7 mwaka huu kwenda Palestina kwa ajili ya
mechi hiyo itakayochezwa Agosti 10 mwaka huu jijini Ramallah. Timu itarejea
Agosti 11 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
» » »

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Julai 25, 2011MECHI YA NGAO YA JAMII (COMMUNITY SHIELD)Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom
2011/2012 kati ya Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe Agosti 13 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, sasa itafanyika Agosti 17 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Uamuzi huo umetokana na timu ya Taifa (Taifa Stars) kuwa na mechi ya kirafiki
katika kalenda ya FIFA (FIFA dates) ugenini itakayochezwa Agosti 10 mwaka huu
dhidi ya Palestina. Stars itarejea nchini Agosti 11 mwaka huu baada ya mechi
hiyo.Wachezaji wengi wanaounda kikosi cha Taifa Stars kwa sasa wanatoka katika klabu
hizo mbili. Awali Stars ilikuwa icheze mechi nyingine Agosti 13 mwaka huu jijini
Amaan wakati aikitokea Palestina. Kocha Mkuu wa Stars, Jan Poulsen ameifuta
mechi hiyo kwa vile Jordan haitakuwa na wachezaji wake wa kulipwa kutokana na
kuwa nje ya kalenda ya FIFA.FAINALI LIGI YA TAIFA
Fainali ya Ligi ya Taifa itakayoshirikisha timu 12 zitakazogawanywa katika
makundi matatu ya timu nne nne itafanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
kuanzia Agosti 6 mwaka huu.
Awali ligi hiyo ilianza katika vituo vinne ambapo timu tatu za juu ndizo
zilizopata tiketi ya kucheza fainali. Kituo cha Pwani kimetoa timu za
Cosmopolitan (Ilala), Sifapolitan (Temeke) na Mgambo Shooting (Tanga) wakati
Samaria (Singida), Majengo SC (Dodoma) na Morani (Arusha) zimefuzu kutoka kituo
cha Singida.
Police Central (Ilala), Small Kids (Rukwa) na JKT Mlale (Ruvuma) zimefuzu kutoka
kituo cha Rukwa wakati kituo cha Kigoma kimetoa timu za Kasulu United (Kigoma),
Geita Veterans (Mwanza) na Rumanyika SC (Kagera).
Timu zinatakiwa kuwasili Tanga siku mbili kabla ya fainali kuanza ambapo mshindi
wa kwanza katika kila kundi pamoja na washindwa bora (best losers) wawili
watapanda hadi daraja la kwanza.Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

» » »

ILIVYOKUWA SIKU YA JUMAPILI MAENEO YA MFALME PUB UROA» » »

KING ABEL NA MY WIFE WAKE NA MTOTO WAOMsanii wa Muziki wa Kizazi Kipya King Abel akiwa na Mkewe pamoja na Mtoto wao walipotembelea Mjengoni

» » »

FFU WA NGOMA AFRIKA BAND WAMERUSHA HEWANI SONGI LA BONGO TAMBARARE

Sunday, July 24, 2011Breaking newzzzzzzz!!!!!!!!!!!!!!
WIMBO WA BONGO TAMBARARE ! UPO HEWANI !!!
FFU wa Ngoma Africa Band waanza
Shamra shamra za miaka 5O ya uhuru mapema!!!!!!!! na kasi kubwa !
Bendi maarufu ya mziki wa dansi baranu ulaya Ngoma Africa band aka FFU,
wamestua ulimwengu kwa kurusha hewani wimbo mpya uliobeba jina la "Bongo
Tambarare" kama mojawapo ya mwanzo wa shamra shamra za kuelekea katika
sherehe za miaka 50 ya Uhuru !
Wimbo huo "Bongo Tambarare" utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda
Ras Makunja,akiimba kwa kushirikiana na Christian Bakotessa aka Chris-B,aka"Mshenzi" wa gitaa la solo,
wimbo unasikika katika kambi ya FFU at www.ngoma-africa.com
wimbo huu ni salam za mwanzo tu kutoka bendi hiyo watanzania wote popote walipo,
lakini bendi hiyo itaipua jikoni vitu vipya rasmi katika siku za usoni,hili kuhakikisha umma wa
wananchi wa Tanzania na marafaki wote wanapata burudani kamili hisiyo na mfano.
usikose kusikiliza "Bongo Tambarare" ya watanzania at www.ngoma-africa.com pia unaweza
ku Log In
» » »

KUOKOTWA KWA MABOMU YA KIVITA NA KULIPULIWANa Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi- Kigoma

Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Maafisa wa JWTZ jana walifanikiwa kulipua mabomu manane na yaliyogundulika kufichwa kwenye kichaka kimoja karibu na Kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Mtabila wilayani Kasulu mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Fraisser Kashai, amesema kuwa mabomu saba kati ya hayo yamegunduliwa na watoto waliokuwa wakichuma matunda katika eneo hilo na baadaye kutoa taarifa kwa uongozi wa eneo hilo na kuwajulisha Polisi wa operesheni na lingine liligundulika katika eneo la bandari ya Kigoma mjini.

Kamanda Kashai amesema kuwa baada ya Polisi kupata taarifa za kuwepo kwa mabomu hayo ambayo yalikuwa yamefichwa kichakani, walifika katika eneo hilo na kubaini kuwa mabomu hayo yalikua hayajalipuka.

Aidha Kamanda amesema kuwa Polisi walipofika katika eneo hilo pia waligundua risari 48 zinazotoa mwanga ambazo zinatumiwa na askari walipo katika mapigano kwenye uwanja wa vita.

Amesema baada ya kubaini hayo yote, Askari hao waliwasiliana na Uongozi wa Polisi Mkoa Kigoma ambapo nao walichukua hatua ya kuwajulisha wenzetu wa Jeshi la Wananchi na kupatiwa wataalamu wa milipuko na kuongozana na Polisi hadi katika eneo la tukio.

Amesema walipofika Maafisa hao walifanya uchunguzi wa kujua aina na uwezo wa mabomu hayo na baadaye kuyalipua kitaalamu na kuepusha madhara.

Kamanda huyo amesema kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani humo, vinaamini kuwa kama mabomu hayo yangelipuka yangeweza kuleta hatari kubwa ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo wakiwemo watoto.

Kwani amesemakuwa kama mabomu hayo yangechezewa ama kukanyagwa kwa bahati mbaya yangeweza kulipuka na kuleta madhara makubwa kwa wananchi.

Amesema Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaendelea kufanya uchunguzi kujua waliohusika na uwekaji wa mabomo pamoja na sisari hizo ili kuwachukulia hatua za kisheria.

Hata hivyo Kamanda Kashai amesema kuwa Vyombo vya Ulinnzi na Usalama mkoani humo kwa pamoja, vimewapongeza wananchi waliotoa taarifa hiyo na kuwaomba wengine kuioga mfano huo kama hatua ya kunusuru maisha ya wananchi wetu kuepuka madhara ya milipuko.

Amewahakikishia wananchi wa eneo hilo na mkoa mzima wakiwemo wakimbiizi kuwa eneo lililogundulika mabomu hayo hivi sasa ni salama na waendelee na shughuli zao kama kawaida na kutosita kutoa taarifa pale wanapobaini kitu wanachokitilia mashaka ili kichukuliwe hatua.

» » »

CHAKA KHAN ATUA DAR, KUFANYA ONESHO JUMAMOSI UBUNGO PLAZA

Thursday, July 21, 2011

Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimkalibisha mgeni wake,Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Marekani,Chaka Khan aliyewasili leo mchana kwenye viunga vya ofisi hizo.Mwanamuziki huyo anatarajia kufanya onesho lake Julai 23 ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza.
habari zaidi nenda HAPA
» » »

MAKACHERO WA POLISI ZANZIBAR WAGUNDUA GHALA LA MIHADARATI

Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi- Zanzibar

Makachero wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamegundua kuwepo kwa nyumba moja inayotumika kama ghala la kuhifadhia na kusambazia mihadarati kwenda kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa visiwani humo.

Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa pamoja na kubainika kwa nyumba hiyo, Makachero hao pia wamewatia nguvuni watu wanne wakiwemo wawili wa familia moja kwa tuhuma za kuhusika na shehena ya mihadarati hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Muhudi Mshihiri, amesema kuwa nyumba hiyo iligundulika huko kwenye eneo la Kiembesamaki karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar

Kamanda Mshihiri amesema kuwa, zaidi ya mafurushi 81 na kiroba cha mbegu za mihadarati vimekamtwa katika nyumba hiyo ambapo mafurushi sita kati ya hayo yalikamatwa kwa mmoja wa wamiliki wa ghala hilo Bakari Maganga Budole(33) wakati akienda kusambazia kwa wauzaji wadowadogo wa biashara hiyo.

Amewataja watuhumiwa wengine walikamatwa kuhusiana na mihadarati hiyo kuwa ni Hamisi Maganga Budole(35), Lusia Toufick Nassoro(28) na Shabani Ibrahim Mhegu(32) wote wakazi wa eneo la Kisimambaazi katika Shehia ya Kiembesamaki mjini Zanzibar.

Kamanda Mshihiri amesema kuwa bado Makachero wake wanaendelea na upelelezi ili kubaini wanakoipata mihadarati hiyo ili kuusambaratisha mtandao mzima.

Amesema kuwa baada ya Polisi wa Kikosi cha Wanamaji na Bandari Zanzibar kuwakamata watuhumiwa wa mihadarati mara kwa mara na kudhibiti uingiaji wake, hivi sasa wafanyabiashara hao hutumia majahazi kwa kusafirishia na kushusha mizigo yao katika maeneo ya Bandari Bubu visiwani hapa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Kikosi cha Wanamaji na Bandari Zanzibar, SP Martin Lisu, amesema bado wanaendelea na utafiti ili kuzibaini bandari zote zisizo rasmi na kuweka mitego ili kuwanasa wale wote wanaojishughulisha na uingizaji wa mali za magendo ikiwemo mihadarati na madawa mengine ya kulevya kutoka viwandani.

Hivi karibuni Polisi wa Kikosi cha Wanamaji na Bandari Zanzibar, waliwakamata watu wawili kwa nyakati tofauti wakiingiza mihadarati visiwani humo kwa kutumia mito ya kulalia na huku mingine ikifungwa kama mahindi ya kuchoma na kuwekwa kwenye viroba.

Hata hivyo Jashi la Polisi limewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa katika vituo vya Polisi pale wanapobaini kuwepo na uhalifu wowote ukiwemo ujambazi wa kutumia silaha na madawa ya kulevya ili wahusika wakamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.

» » »

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 21, 2011

SHELISHELI KUWASILI ARUSHA KESHO
Timu ya Taifa ya Shelisheli inatarajia kuwasili Arusha kesho mchana (Julai 22
mwaka huu) ikitokea Nairobi kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23.


Mechi hizo zitachezwa Julai 27 na 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sheikh Amri Abeid Kaluta, jijini Arusha. Mechi zote zitaanza saa 10 jioni. U23
ambayo iko kambini Dar es Salaam chini ya kocha wake Jamhuri Kihwelo itaondoka
Jumapili kwenda Arusha kujiandaa kwa mechi hizo.

Shelisheli inakuja na msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 24. Wachezaji ni
Nelson Sopha, Vincent Euphrasie, Jonathan Bibi, Nigel Freminot, Allen Larue,
Ronny Marengo, Gervais Waye Hive, Achille Henriette na Karl Hall.

Wengine ni Alex Nibourette, Jude Nancy, Jones Joubert, Alpha Balde, Nelson
Laurence, Trevor Poiret, Henny Dufrene, Don Anacoura, Kevin Betsy, Brian Dorby,
Wilnes Brutus, Eugene Valentin, Rashim Padayachy, denis Barbe na Damien Maria.


U23 itaondoka Julai 25 mwaka huu kwenda Arusha ikiwa na kikosi cha wachezaji 20.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewaongeza kwenye U23 wachezaji Juma
Seif Kijiko wa Yanga, Haruna Moshi wa Simba na Gaudence Mwaikimba ambaye msimu
huu ameombwa usajili Moro United.

Lengo la Poulsen ni kuangalia kiwango cha wachezaji hao ili kuona kama anaweza
kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho Agosti 10 mwaka huu kitacheza
na Palestina katika mechi ya kirafiki itakayofanyika jijini Ramallah. Poulsen
atataja kikosi hicho Julai 31 mwaka huu jijini Arusha baada ya mechi hizo mbili.

Pia Kihwelo ametaja kikosi cha wachezaji watakaokwenda Arusha. Wachezaji hao ni
Shabani Kado (Yanga), Seif Abdul (African Lyon), Juma Seif (Mtibwa Sugar), Babu
Ally (Morani), Shomari Kapombe (Polisi Morogoro), Issa Rashid (Mtibwa Sugar),
Salum Kanoni (Simba), Godfrey Wambura (Simba), Jabir Aziz (Azam) na Juma Seif
Kijiko (Yanga).

Wengine ni Awadh Juma (Mtibwa Sugar), Haruna Moshi (Simba), Mohamed Soud (Toto
Africans), Salum Machaku (Simba), Salum Mnyate (Azam), Khamis Mcha (Azam),
Thomas Ulimwengu, Gaudence Mwaikimba (Moro United0, Sino Augustino (African
Lyon) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).

MUSA MGOSI, MOTEMA PEMBE
Daring Club Motema Pembe (DCMP) ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kupitia
Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu vya nchi hiyo (FECOFA) limetuma TFF
maombi ya Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mshambuliaji wa
Simba, Musa Hassan Mgosi.

Klabu hiyo imemuombea Mgosi hati hiyo ya uhamisho kama mchezaji wa ridhaa kwa
maelezo kuwa imeshakubaliana na wenzao wa Simba katika suala hilo. Hivyo hivi
sasa TFF inafanya mawasiliano na Simba kabla ya kufikia uamuzi wa kutoa ITC kwa
DCMP.

USAJILI WA WACHEZAJI 2011/2012
Klabu zote 14 za Ligi Kuu ya Vodacom zimewasilisha usajili wa wachezaji wao kwa
ajili ya ligi hiyo iliyopangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu. Mechi
ya kuzindua msimu kati ya Simba na Yanga itachezwa Agosti 13 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.

Muda wa mwisho kuwasilisha usajili ilikuwa saa 6.00 usiku Julai 20 mwaka huu.
Klabu zote ziliwasilisha usajili wao Julai 20 mwaka huu kwa wakati na muda
waliowasilisha ukiwa ndani ya mabano.

Klabu hizo ni Ruvu JKT Stars (saa 9.00 alasiri), Oljoro JKT (saa 9.00 alasiri),
Kagera Sugar (saa 9.00 alasiri), Ruvu Shooting (saa 10.00 jioni), Polisi Dodoma
(saa 10.30 jioni), Moro United (saa 10.45 jioni), Simba (saa 1.30 usiku), Azam
(saa 3.45 usiku), African Lyon (saa 4.30 usiku), Yanga (saa 4.30 usiku), Villa
Squad (saa 5.30 usiku), Mtibwa Sugar (saa 5.40 usiku), Toto African (saa 5.50
usiku) na Coastal Union (saa 5.58 usiku).

Ofisa Habari
Boniface Wambura
» » »

MAREKANI YAFURAHISHWA NA VIJANA ZANZIBAR

Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso wakati alipofika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Ferej ofisini kwake Migombani na baadae kutembelea sober house ya mwanzo iliyoko Tomondo iliyoanzishwa 13/01/2009.

MAREKANI imefurahishwa na dhamira ya vijana kujiunga na vituo vya huduma kwa vijana walioachana na madawa ya kulevya visiwani Zanzibar na kusema hatua hiyo ni mafanikio ya vita dhidi ya biashara ya madawa hayo.

Msimamo huo ulionyeshwa jana na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt alipotembelea kituo cha Tomondo Sober House, kinachotoa huduma kwa vijana walioachana na utumiaji wa madawa ya kulevya katika eneo la Tomondo, mjini hapa.

“Uamuzi wenu wa kijiunga na vituo hivi, ni njia sahihi zaidi katika vita vya kupambana na bishara ya madawa ya kulevya duniani, kwa sababu hatimaye bishara hiyo itakosa soko,” alisema Balozi Lenhardt.

Aliambiwa kuwa zaidi ya vijana 300 walioachana na tabia ya kutumia madawa ya kulevya wamepitia katika kituo cha Tomondo Sober House na kupatiwa huduma mbali mbali na kwamba asilimia 30 kati ya hao sio mateja tena baada ya kurejea katika maisha ya kawaida.

Tomondo Sober Haouse ni miongoni mwa vituo vitano vinavyotoa huduma ya aina mbali mbali ikiwemo elimu kwa vijana waliachana na madawa ya kulevya katika visiwa wa vya Unguja na Pemba .

Akifafanua msimamo wa Marekani katika vita dhidi ya biashara ya kulevya Balozi Lenhardt alisema nchi yake inaamini kuwa njia sahihi ya kufanikisha vita hiyo ni kuua soko la madawa ya kulevya kwa watumiaji kuachana na tabia hiyo.

“Tunahitaji vijana zaidi kama ninyi, wanaume na wanawake kujitokeza kuachana na madawa ya kulevya, sisi kama nchi tutasaidia kuwaelimisha wasitumie madawa, na wauzaji pia wataacha kuleta madawa Zanzibar ,” alisema Balozi Lenhardt.

Alisema ingwa uamuzi wa kuachana na madawa ya kulevya ni mgumu, lakini kwa dhamira inawezekana na kutoa mfano wa kaka yake kwamba alifanikiwa kuachana na tabia hiyo baada ya kutumia madawa ya kulevya kwa zaidi miaka 35 na sasa sio mwathirika tena.

Alisema anaamini inawezekana kwa vijana wengi zaidi Zanzibar kuachana na tabia hiyo kwa sababu: “Mnajua namna kulinda maisha yenu, lakini madawa ya kulevya hayana uwezo wa kukulazimisheni kuyatumia ikiwa mumeamua kuacha.”

Mapema Balozi lenhardt alikuwa na mazungumzo na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Zanzibar , Fatma Abdulhabib Fereji huko Migombani nje kidogo kutoka mjini hapa.

soma zaidi HAPA

» » »

MMOJA ASHIKILIWA NA POLISI KIGOMA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MKEWE

Tuesday, July 19, 2011

Na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi Kigoma

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Nkundusi katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Yohana Adam Sabuni(28), anashikiliwa na Polisi mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya mkewe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7.00 huko katika kijiji Nkundusi wilayani Kasulu, mtuhumiwa Yohana alimshambulia mkewe Bi. Roziana Fidelis Pahida(26), kwa kutumia mpini wa jembe na mianzi hadi kumuua.

Kamanda Kashai amesema kuwa mara baada ya mtuhumiwa huyo kubaini kuwa mkewe ameshafariki, alianza kukimbia kwa lengo la kukwepa kesi na ndipo Polisi walipopata taarifa kutoka kwa raia wema ambapo walimfuatilia na kumtia nguvuni.

Amesema kuwa kutokana na kipigo hicho, marehemu alipasuka bandama na kusababisha kutokwa na damu nyingi zilizopelekea kifo chake.

Kamanda huyo wa Polisi mkoa wa Kigoma amesema uchunguzi wa awali wa tukio hilo unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo kinatokana na hisia za wivu wa kimapenzi ambapo marehemu aliondoka nyumbani kwake na kuomba hifadhi nyumba jirani baada ya kuona kuwa mumewe kachelewa kurudi naye kuhofia kulala peke yake.

Kamanda Kashai, amesema baada ya mtuhumiwa kurejea nyumbani usiku huo na kubaini mkewe hayumo ndani, ambapo baada ya muda, marehemu alisikia sauti ya mumewe akiimba akirudi kutoka ulevini na ndipo alipotoka kwa jirani na kurudi kwake kitendo ambacho kilimkasirisha mtuhumiwa na kuona kuwa labda alikuwa akifanya mapenzi na jirani yake.

Amesema hatua hiyo ilimfanya mtuhumiwa huyo kumshambulia mkewe jambo ambalo sio tu kuwa lilikuwa ni la kikatili, bali pia ni kitendo kinyume na haki za binadamu na udharimu wa unyanyasaji wa kikatili dhidi ya wanawake na watoto mambo ambayo pia yanapingwa vita na Umoja wa Mataifa.

Amesema kuwa, mume au mke apatwapo na matatizo na mwenziwake anatakiwa kwenda Kituo cha Polisi ambapo kuna Madawati maalumu ya kushughulikia matatizo ya wanawake na watoto na kupatiwa ufumbuzi au ushauri wa matatizo yao.

Kamanda Kashai amesema kuwa tayari Polisi wameanza upelelezi ikiwa ni pamoja na kumhoji Mtuhumiwa na baadaye atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya kuchukua sheria mkononi kwani kwa kufanya hivyo ni kujitafutia matatizo ambayo yatamfanya akamatwe na Polisi na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili na hata kufungwa Jeshia.
.............................................................
Source: Insp. Mohammed Mhina, Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar.
» » »

NGOMA AFRICA BAND WASHAMBULIA TüBEINGEN FESTIVALl ! UJERUMANI
FFU wa Ngoma Africa band wakiwa katika mashambulizi! Tübingen Festival,
Mabakuli ya "Supu ya Mawe" yawalewesha washabiki !
Kile kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU,siku ya jumamosi ya 16.7.2011
kilijikuta kikiwa na kazi moja tu...ya kuwachanganya akili washabiki katika onyesho kubwa la African Internationals Festivals ,lilofanyika mjini Tübingen,ujerumani.

Bendi hiyo maarufu barani ulaya ilijukuta ina kibarua sugu cha kuwapeleka puta maelfu ya washabiki waliokuwapo katika uwanja wa dansi, FFU hao wa muziki walifanikiwa kuwachanganya washabiki wao kwa kutumia mdundo na mlindimo wa muziki..ambapo
washabiki walijikuta hawana nafasi ya kupumua...mbele ya dansi la Ngoma Africa,
Kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja alikiongoza kikosi chake chenye
washambuliaji akina Chri-B,wanadada wawili akina Beda Beraca aka Princess Bedi Bella ,na Severn Okomo,safi ya magitaa wakiwemo Maxime Buanda,Matondo na mkali wa solo Chris-B aka "mshenzi",Willy Mbiya katika kukaanda Drum.

Tafadhali usikose kupiga chabo au kupata bakuli la "Supu ya Mawe" at www.ngoma-africa.com


Mshambuliaji wa kike wa Ngoma Africa band,Princess Bedi Beraca aka Bedi Bella akishambuli jukwaani nyuma yake mwenye mtutu ni Chris-B aka "Mushenzi" wa solo gitaa.
» » »
Newer Posts Older Posts

UNAPOHITAJI kujua DUNIANI nini kimetokea, Basi fuatilia Kurasa Zangu za Kijamii TWITTER, FACEBOOK pamoja na INSTAGRAM, BONYEZA hapa >>> TWITTER, INSTAGRAM na FACEBOOK, PIA Unaweza Kujiunga na chaneli yangu ya YOUTUBE, ili kutazama Video >>>YOUTUBE

 

Copyright © 2010 NYUMBANI KWANZA. All Rights Reserved.