-->

UHOLANZI KUZIDISHA UHUSIANO NA USHIRIKIANO NA ZANZIBAR KUIMARISHA SEKTA YA UTALII

Tuesday, October 30, 2012

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

    Zanzibar   30.10.2012


UHOLANZI imeeleza azma ya kuzidisha uhusiano na ushirikiano kati yake na Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii na kusisitiza kuwa tayari mashirika ya ndege kutoka nchini humo likiwemo Shirika la ndege la KLM yameonesha nia ya kufanya safari zake moja kwa moja kutoka Uholanzi hadi  Zanzibar.


Balozi wa Holland nchini Tanzania Mheshimiwa Dk. Ad  Koekkoek  aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar.


Katika maelezo yake Balozi Koekkoek alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania ikiwemo Zanzibar na kuahidi kuukuza na kuuendeleza hasa katika sekta mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo utalii. 


Balozi huo alieleza kuwa ili kuhakikisha ushirikiano huo wa pande mbili hizo unadumishwa  alisisitiza haja hiyo ya kuwepo kwa usafiri wa moja kwa moja wa anga kutoka Holland mpaka Zanzibar hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza sekta ya utalii na hata sekta ya biashara.


Aidha, Balozi huyo alieleza kufarajika kwake kwa kuwepo uhusiano na ushirikiano kati ya Zanzibar na Uholanzi ambao unazidi kuimarika siku hadi siku.


Katika mazungumzo hayo Balozi Koekkoek  alimueleza Dk. Shein kuwa amefurahishwa sana na juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendeleza sekta hiyo ya utalii nchini.


Alisema kuwa Zanzibar imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii hatua ambayo imepelekea kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka kila pande ya dunia ikiwemo nchi ya Uholanzi.


Kutokana na hatua hiyo Balozi  Koekkoek ameeleza kuwa ipo haja ya kuzidisha uhusiano katika sekta ya utalii hasa ikizingatiwa kuwa na ushindani mkubwa katika sekta ya utalii katika nchi za visiwa vidogo vidogo.


Kwa upande wa sekta ya biashara Balozi huyo alimueleza Dk. Shein kuwa wafanya biashara kutoka Uholanzi wamevutiwa na fursa kadhaa za kuekeza zilizopo Zanzibar ambazo zitawarahisishia kuwekeza.


Balozi  Koekkoek alieleza kuwa juhudi na azma ya Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kuipandhisha daraja hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa hospitali ya rufaa hi za kupongezwa.


Hivyo ameahidi kuwa nchi yake itaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa hatua mbali mbali ambapo hivi sasa teyari mikakati kadhaa imeshawekwa ya kuhakikisha ufanikishaji wa suala hilo.


Balozi huyo alieleza kuwa Zanzibar imekuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali za bahari hivyo kuna umuhimu wa kulindwa na kuhifadhiwa  huku  akiipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua mbali mbali inayochukua katika kuhifadhi  rasilimali hizo na kueleza haja ya kukuza na kuimarisha ushirikiano katika sekta hiyo muhimu.


Kwa mara nyengine tena Balozi  huyo alitoa mkono wa  pole kwa ajali ya kuzama kwa meli ya MV.Skagit iliyotokezea Julai mwaka huu na kusababisha maafa makubwa yaliyopelekea kwa vifo kwa raia wengi wa Tanzania na wageni kutoka nje ya Tanzania.


Balozi  huyo alitoa shukurani zake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano alioupata katika kuhakikisha raia wa Uholanzi ambao waliokuwemo katika ajali hiyo katika upatikanaji wa taarifa na kuwashughulikia vyema.


Naye  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein  alitoa shukurani zake kwa nchi ya Uholanzi kutokana na kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi hiyo na Zanzibar ambao ni wa muda mrefu na umeweza kuleta maendeleo kwa pande zote mbili.


Dk. Shein alielzea uzoefu wake alioupata wakati akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi Uholanzi iilivyokuwa ikiunga mkono Tanzania katika nyanja mbali mbali za maendeleo  hatua ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta hizo za maendeleo endelevu kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kwa upande  wa sekta ya utalii Dk. Shein alitoa pongezi kwa Balozi huyo binafsi na kwa nchi yake kwa azma alionayo katika kuimarisha mashirikiano katika sekta hiyo na kueleza furaha yake juu ya azma ya kuanzishwa kwa usafiri wa anga wa moja kwa moja kati ya Uholanzi na Zanzibar  hatua ambayo itasaidia kuongeza idadi ya watalii nchi na kuinua pato la taifa nchini.


Dk. Shein aliipongeza azma ya Uholanzi ya kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kuiimarisha hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ambayo yote hayo ni miongoni mwa malengo ya Serikali ya Mapainduzi Zanzibar.


Kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira ya bahari Dk.Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar itaendeleza  juhudi zake katika uhifadhi wa mazingira na kutoa shukurani kwa ushirikiano unaotolewa na Uholanzi kwa Zanzibar katika uhifadhi wa mazingira hayo.


Hata hivyo, Dk.Shein alieleza kuwa katika kuhakikisha usalama wa usafiri wa bahari unaimarishwa zaidi mashirikiano makubwa ya Mamlaka za bahari kati ya Zanzibar na Tanzania Bara zikiwemo SUMATRA na ZMA zinaimarishwa.


Dk. Shein alieleza kuwa  mbali ya juhudi hizo zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha usalama wa bahari unaimarika  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika mchakato wa ununuzi wa meli mpya ambayo itasaidia katika usafiri wa baharini hasa kwa wananchi wenye kipato cha chini.


Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza kufarajika kusikia azma ya wawekezaji kutoka Uholanzi kuja kuwekeza Zanzibar na aliwaahidi kuwa Zanzibar itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji.


Sambamba na hayo, Dk. Shein alimuhakikishia Balozi huyo kuwa amani na utulivu iliyopo nchini itaimarishwa. 

VOA: KIMBUNGA SANDY KINASABABISHA HASARA KUBWA MAREKANI

Rais Barack Obama atangaza majimbo ya kaskazini mashariki ya Marekani ya New York na New Jersy kuwa maeneo ya "maafa makubwa" kufuatia kimbunga kikubwa kilichopewa jina la Sandy kusababisha mafuriko na uharibifu mkubwa katika majimbo hayo.

Tangazo hilo lililotolewa Jumanne linaruhusu kutumiwa fedha za serikali kuu za kukabiliana majanga kutumiwa ili kusaidia juhudi za kukabiliana na maafa katika majimbyo hayo.

Kimbunga Sandy kilifika nchi kavu siku ya Jumatatu jioni na kinaendelea kupunguka nguvu zake kinapita sehemu za kati na kaskazini ya marekani. Maafisa wanasema watu 16 walifariki katika katika maeneo ya mashariki ya Marekani kutokana na kimbunga hicho ambacho kilisababisha vifo vya watu 65 wiki iliyopita katika nchi za Caribbean.

Kwa siku ya pili mfululizo shughuli zote za serikali na biashara pamoja na shule katika miji mikubwa mashariki ya Marekani ziliendelea kufungwa siku ya Jumanne wakati mamilioni ya watu wakiwa hawana huduma ya umeme.

Takriban wasafiri elfu 10 walikwama katika miji hiyo ya mashariki ya nchi baada ya maelfu ya safari za ndege kuahirishwa kwa siku ya pili. Halikadhalika huduma za usafiri wa mijini iliendelea kufungwa na mjini New York kumekuwepo na mafuriko ya maji katika njia za reli za chini kwa chini.

Watalamu wa uchumi wanatabiri kwamba kimbunga Sandy huwenda kimesababisha hasara inayogharimu  takriban  dola bilioni 20.

MAALIM SEIF: VIKOSI VYA ULINZI BARA NA VYA SMZ VINAHITAJI KUPATIWA MAFUNZO YA ZIADA KUKABILIANA NA VURUGU

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema vikosi vya ulinzi vya Tanzania na vile vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vinahitaji kupatiwa mafunzo ya ziada juu ya kukabiliana na vitendo vya vurugu na kulinda amani ya nchi.

Amesema vikosi hivyo vimekuwa vikitumia nguvu za ziada katika kukabiliana na vitendo hivyo, hali inayopelekea kuleta madhara kwa raia wasiokuwa na hatia pamoja na mali zao.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliofika kwa ajili ya kubadilishana mawazo.

Ameeleza kuwa mara nyingi vikosi vya ulinzi vya Tanzania vimekuwa vikifanya kazi kwa kufuata matakwa ya wanasiasa na kusahau mwongozo na maadili ya kazi yao, huku vikosi vya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vikifanya kazi bila ya kuwa na taaluma ya kutosha, na kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuleta mabadiliko ya kiutendaji ndani ya vyombo hivyo vya ulinzi.

Kwa upande mwengine Makamu wa Kwanza wa Rais ameelezea haja ya kulifanyia mapitio daftari la kudumu la wapiga kura ili liweze kwenda na wakati.

Amesema ucheleweshaji wa kulifanyia mapitio daftari hilo unaweza kusababisha baadhi ya wananchi kukosa haki yao ya kupiga kura baada ya kutimiza masharti na sifa za kuwa wapiga kura.

“Daftari hili linatakiwa kufanyiwa mapitio kila mwezi wa Oktoba lakini hadi sasa halijapitiwa, na sidhani kuwa kuna mpango huo kwa sasa”, alikumbusha Maalim Seif.

Hata hivyo amesema huenda tatizo hilo limetokana na ukosefu wa fedha, na kusisistiza haja kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kufanya kazi kwa uwazi ili kujenga matumaini kwa wananchi.

“Ukweli ni kwamba tunahitaji kuwa na chaguzi huru na za haki katika nchi yetu, na hali halitowezekana kama Tume ya Uchaguzi haitofanya kazi kwa uwazi ‘transparent’”, alitanabahisha.

Akizungumzia kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Maalim Seif amesema inafanya kazi vizuri licha ya changamoto ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa baadhi ya watendaji hasa katika ngazi ya Shehia.

“Huku juu tunashkuru kwamba tunakwenda vizuri, lakini mgawanyo wa madaraka uko katika ngazi ya Mawaziri tu. Kinachojitokeza ni kuwa bado baadhi ya watendaji wa ngazi za chini hawajataka kubadilika hasa masheha” alifahamisha na kuongeza,

“Mfumo huu wa serikali ya umoja wa kitaifa ndio unaotufaa kuliko mfumo wowote ule kwa Zanzibar kwa sababu umewaunganisha Wazanzibari na ndio walioamua kuwa na mfumo huo”, aliongeza.

Akijibu hoja za wajumbe hao waliotaka kujua juu ya nafasi ya mwanamke wa Zanzibar kuhusu siasa, Makamu wa Kwanza wa Rais amesema Serikali inafanya juhudi za kuwashajiisha wanawake kugombea nafasi za uongozi badala ya kusubiri nafasi za uteuzi pekee.

Kwa upande wake kiongozi wa ujumbe huo Bw. Akinyemi Adegbola ambaye ni msaidizi wa masuala ya uchaguzi wa Umoja wa Mataifa kutoka makao makuu New York, amesema Umoja huo utaendelea kuzifanyia kazi changamoto  mbali mbali zinazojitokeza kwa nchi wanachama zikiwemo zile zinazohusiana na masuala ya uchaguzi.

Hassan Hamad (OMKR).

SIKILIZA FLEVA 145 ZA LEO HAPA

Monday, October 29, 2012

FLEVA 145 COCONUT FM OCTOBER 29 2012

PINKY XXX ATAMANI KUFANYA NGONO NA MYSTOKAL
KATIKATI ya Mwezi October Baada ya Mystical kutaja Jina la Pinky kuwa Ndo Chaguo lake katika Porn, Hatimaye Pinky Amefunguka na Kusema Anatamani apate kufanya naye Scene ya Porn. Sarah Mira Belli maarufu kwa Jina la PINKY XXX huyu ni Binti Aliyejizolea Umaarufu kwa Kucheza Picha Za NGONO na Sasa bado hajakata tamaa katika Mpango wake wa Kushiriki Picha ya Utupu na Mwana HIP HOP toka YMCMB, MYSTICAL na ameeleza ni Kitu gani FANS ambacho watakiona Kama Mpango wake huo Utakaa Sawa. "Ningependa kushiriki na Mystikal, especially kwa Matumizi ya Website yangu, Lakini endapo zitajitokeza Kampuni kutuomba wakiwa na Pesa za Kutosha, nitafanya Hivyo mradi tu Watimize matakwa yangu! Sijajua kama Mystikal ataperfome Vizuri Kitandani, Siwezi kusema... Sijui! baadhi ya Mitindo ambayo ningependa Kufanya na Mystikal katika Scene, ni mitindo iliyozoeleka na ambayo huwa natumia katika Scene Zangu, kama Vile.. doggyStyle, Spoon, na Froggy possition" Alisema Pinky wakati Akiongea na Vlad TV.
 
MZIGO MPYA "NATAKA KULEWA" WA DIAMOND UMEDONDOSHWA LEO
Ngoma Mpya ya Diamond "Nataka Kulewa"
 

NATINA REEDS DIED TWO DAYS BEFORE HER 33 BIRTHDAY
Natina Tiawanna Reed (October 28, 1979 – October 26, 2012) Died on October 27, 2012, one day shy of her 33rd birthday, in a car accident as she was walking on a state highway in Atlanta, Georgia. At the time of her death, Reed had been working on a solo rap album, as well as a new movie and reunion with fellow members of Blaque. The accident happened at about 10:30 p.m. near Lawrenceville, Georgia on U.S. Highway 29 near Hamilton Road. 

No charges are expected, said Gwinnett police. Police and firefighters arrived to find a bystander performing CPR on Reed at the scene. She was pronounced dead a short time later at Gwinnett Medical Center. A preliminary investigation indicates that Reed was in the roadway when she was struck. Only the vehicle's driver and a passenger witnessed the impact.

 The driver of the vehicle was determined to be not at fault, and there are no charges pending. In 2001, Reed was engaged to rapper Kurupt. In 2002, she gave birth to their son Tren Brown after the group was dropped from their label. Reed and Kurupt were separated. Reed was the cousin of former Destiny's Child member Farrah Franklin.
 

LEXA MMOJA WA WATENGWA ACHOMWA KISU NA KUFARIKI
Juzi ijumaa ya tarehe 26 october nilipokea sms nyingi zikinitaka kufafanua na wengine kuniuliza kama habari zinazohusu kifo cha memba wa atengwa anaeitwa Lexa ni kweli ama si kweli..sasa kwa habari nilizonazo ni kuwa info hizo ni za kweli na ilitokea siku ya ijumaa ambapo alikabwa na kunyang'anywa vitu vyake na watu wanaomfaham na kisha kumchomwa kisu Soma hapa Zaidi DJ FETTY


SOLANGE KNOWLES AJA NA VIDEO MPYA
SOLANGE KNOWLES ametangaza Ujio wa ALBUM yake MPYA inayojulikana Kwa Jina la "TRUE" Solange ambaye Pia ni Mdogo wake Beyonce Knowles, Amekua Kimya long time, lakini Ameamua Kuvunja Ukimya Kwa kurelease VIDEO ya Wimbo wake Mpya Unaoitwa "LOSING YOU" ikiwa ni Video ya Wimbo unaoitambulisha Album yake. Album Imejuimuisha SONGZ mbalimbali na Itakuwa Chini ya Usimamizi wa Terrible Records, na Inategemewa Kuingia Sokoni November 27, 2012. Solange, Amewataka FANs wake Woote wajue She's BACK wakae tayari for NEW ALBUM.

TAARIFA ZA MICHEZO KUTOKA TFF

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 29, 2012
 
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA SHIREFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu).
 
Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SHIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Shinyanga.
 
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SHIREFA ambayo imechaguliwa chini ya uenyekiti wa Benester Lugora.
 
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu Shinyanga kwa kuzingatia katiba ya SHIREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
 
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
 
Viongozi waliochaguliwa ni Benester Lugora (Mwenyekiti), Nassoro Said (Katibu Mkuu), Bivin Kapufi (Katibu Msaidizi), Mbasha Matutu (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF) na Michael Kaijage (Mwakilishi wa Klabu TFF).

HABARI LEO: BABU WAMBAKA MJUKUU WAO

MTOTO wa miaka 11 aliyekuwa anasoma Darasa la Sita katika Shule ya Msingi ya Mbezi wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, amedaiwa kubakwa na babu zake wawili wenye umri wa zaidi ya miaka 50.

Kutokana na hali hiyo, mama wa mtoto huyo (wote majina tunayo), anatishiwa maisha na ndugu wa mwanamume aliyezaa naye baada ya kutoa siri za kubakwa kwa mtoto huyo.

Mama huyo amedai kutaka kugeuziwa kesi baada ya kushitaki polisi vitendo vya ubakaji alivyofanyiwa mwanawe na babu zake wawili wa upande wa baba anaodai wana umri zaidi ya miaka 50 kwa nyakati tofauti, Julai na mapema mwezi huu (Oktoba).

Akizungumza na gazeti hili jana, mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kufanyiwa vitendo hivyo na babu zake wawili, mkazi wa Mbezi, Malamba Mawili, Dar es Salaam, alidai mwanawe alibakwa na alipoamua kuchukua hatua polisi, sasa anatishiwa na ndugu wa mwanamume.

“Mwanamume niliyezaa naye mtoto huyo (jina tunalo) tuliachana, mwezi mmoja uliopita akaja kumfanyia uhamisho mtoto kwenda Gongo la Mboto anakoishi kwa vile mtoto ana zaidi ya miaka saba, sikukataa niliposikia japo hakunishirikisha, lakini tangu amemhamisha mpaka leo shule hajaanza,” alisema mama huyo na kuongeza: “Wiki mbili zilizopita, nilipigiwa simu na baba wa mtoto wangu kuwa mtoto ametoroka, nikaenda na tukatoa taarifa Kituo cha Polisi Gongo la Mboto, niliporudi nyumbani kesho yake, wakanipigia amepatikana kwa babu yake mdogo katika familia ya babu mzaa baba yake, wakiniomba niende tukaongee maana kuna jambo limetokea.”

Mama huyo alisema alipokwenda, alikuta kuna kikao cha ndugu wa mwanamume na walianza kumwomba radhi wakimueleza kuwa mtoto alitoroka baada ya kuingiliwa kimwili na babu ndugu wa familia (jina tunalo) na walimtaka wamalize suala hilo kifamilia.

“Mtoto alipohojiwa alikiri kweli kubakwa na babu huyo na walisisitiza nisamehe huku wakimtaja Mungu, lakini mimi nikasema hilo ni kosa la jinai, tulipotoka nikaenda Polisi Mbezi kwa Yusuf ili mtoto ahojiwe na kisha hospitali ya Serikali ya Mbezi kumpima mwanangu,” alidai mama huyo.

Alisema vipimo vya hospitali vilihakikisha kweli mtoto alibakwa, lakini akawa hana ujauzito wala Ukimwi na mtoto alipohojiwa polisi, alikiri kubakwa na kueleza kuwa vitendo hivyo alikuwa akifanyiwa pia na babu mdogo wa mwisho kwa babu yake Julai mwaka huu.

“Kinachonisikitisha ni kwamba, yule mgambo aliyenisaidia kuwapata watuhumiwa hadi kuwafikisha polisi, sasa amekamatwa na watuhumiwa wapo huru, kama haitoshi, ndugu wa mwanamume wananitumia ujumbe wa simu wa kunitishia kuwa watahakikisha wananigeuzia kesi, naomba Serikali inisaidie katika hili,” alilalamika mama huyo.

Alisema pia Polisi wamekuwa wakimpiga danadana kuhusu suala hilo akiwafuata kuulizia hivyo kutokana na vitisho vya ndugu wa mwanamume wanaodai watamshikisha adabu kwa kuwa ameidhalilisha familia yao kushitaki suala hilo polisi wakati wangelimaliza kifamilia, anaishi kwa wasiwasi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alipoulizwa jana kuhusu tukio hilo, alisema hana taarifa, lakini alisema Polisi inawezekana wanafanya upelelezi ndio maana hawana jibu la moja kwa moja kwa mama huyo kiasi cha kuona anazungushwa na kumuomba aende ofisini kwake leo.

“Naomba kama anahisi anazungushwa au kuonewa, aje ofisini kwangu kesho (leo), unajua kesi kama hizi zinahitaji upelelezi, pande zote mbili lazima watafute ukweli, siwezi kusema sana maana sijafikishiwa tukio hili kwangu ila kama anaona mambo hayaendi aje,” alisema Kenyela.

Baba mzazi wa mtoto huyo alipotafutwa kwa simu ya mkononi, namba yake ilikuwa ikiita bila kupokewa na baadaye mtu mwingine alizungumza na mwandishi, kumweleza kuwa simu ya baba huyo ni mbovu.

MATATIZO MENGI YA WANANCHI WA VIJIJI VYA BWELEO NA BWEFU YAMEPATA UFUMBUZI KUTOKANA NA WIVU WA MAENDELEO BILA KUWATEGEMEA WAHISANI: BALOZI SEIF

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wivu waliokuwa nao Wananchi wa Vijiji vya Bweleo na Bwefumu viliopo Wilaya ya Magharibi wa kujiletea Maendeleo ndio uliosababisha matatizo yao mwengi kupata ufumbuzi bila ya kutegemea nguvu za wahisani.

Balozi Seif alisema hayo mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja katika Vijiji hivyo kuangalia harakati zao za Maendeleo pamoja na kutambua changamoto zinazowakabili  ndani ya Viji vyao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mfano huo wa wivu wa Maendeleo  ndani ya Bweleo na Bwefumu ambao ni nadra kufanywa na Jamii nyingi  alishauri kuwa chachu kwao na Vizazi vijavyo.

Alisema Mataifa mengi  Duniani akayatolea mfano wa China na Japani yamefanikiwa kwa kutumia mfumo huu wa kushindana katika maendeleo ndani ya Majimbo na Maeneo yao.

“ Ukiiangalia Jahumuri ya Watu wa China kila Jimbo ndani ya Nchi hiyo imekuwa na  shirika lake la ndege kitendo mfumo ambao umesaidia kunyanyuka kwa haraka kwa uchumi wa Mjaimbo hayo na China yenyewe kwa ujumla”. Alisisitiza Balozi Seif.

Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alifahamisha kwamba katika kukabiliana na tatizo sugu la ukosefu wa huduma ya Maji safi na salama katika Kijiji cha Bweleo alisema serikali tayari imeshatoa hundi ya shilingi Milioni  Hamsini na  Nane { 58,000,000/- } kwa ajili ya kuondosha tatizo hilo.

Alisema fedha hizo zimeelekezwa kugharamia kuungwaji wa Mashine na Bomba za maji kutokla Kisima cha Maji kiliopo Dimani ambapo Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar umeshaahidi kwamba kazi hiyo itakamilika ndani ya kipindi cha Mwezi Mmoja baada ya kupatikana kwa Feha hizo.

Kuhusu miradi ya Maendeleo ya Vijiji hivyo Balozi Seif katika Kuunga Mkono juhudi za Wananchi hao ameahidi kutoa mchango wa Shilingi Milioni moja           { 1,000,000/- } kupiga plasta Jengo la Skuli ya Maandalizi ya Bweleo na shilingi Milioni Moja na Nusu { 1,500,000/- } kukamilisha ujenzi wa sehemu ya kulitia udhu katika Msikiti Kuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Bweleo.

Balozi Seif alisisitiza umuhimu wa Elimu na kuwaomba wazazi wa Vijiji hivyo kuendelea kuwekeza Watoto wao katika Sekta ya elimu ambayo ndio itakayowakomboa ndani ya mfumo wa sasa wa Dunia ya Teknolojia.

“ Tumeshuhudia Baadhi ya Wazazi kuwekeza mali zao katika Mashamba, Nyumba na Hata Vipando vya usafiri lakini matokeo yake anaacha vurugu, matatizo kwa kizazi chake wakati wa urithi”. Alifafanua Balozi Seif.

Katika Risala yao iliyosomwa na Mmoja wa Wananchi hao Ndugu Mussa Shaali Choum Wananchi hao walielezea wasi wasi wo kutokana na fujo na vurugu zinazoendelea kutokea katika baadhi ya maeneo hapa Nchini.

Wananchi hao walisema tabia hiyo inayofanywa na baadhi ya Vijana kwa kivuli cha  cha Jumuiya ya Uamsho inaleta sura mbaya na ni tabia inayofaa kupigwa vita na jamii yote kwa vile inahatarisha amani ya Nchi.

Katika Ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikagua Skuli ya Bwefumu na kushuhudia baadhi ya majengo ya skuli hiyo yakiwa katika hali ya uchakavu hasa mapaa yake.

Balozi Seif aliuagiza Uongozi wa Jimbo la Dimani kutumia fedha za Mfuko wake wa Jimbo katika kufanya matengengezo ya mapaa ya majengo hayo badala ya kusubiri Wizara husika ambayo imekabiliwa na majukumu manengi.

Balozi Seif pia alikagua eneo la majengo ya Kihistoria ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefi kati ya Wananchi wa Vijiji hivyo pamoja na Muwekezaji aliyepewa eneo hilo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  aliahidi kwamba Serikali Kuu itafanya uchunguzi wa kina na baadaye kutoa uamuzi unaostahiki kuhiana na eneo hilo baada ya kujitokeza ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uwekezaji hapa Nchini.

Baadaye Balozi Seif aliangalia Bandari ya Bweleo ambayo Wavuvi wa eneo hilo huitumia kwa shughuli za uvuvi, Mwani pamoja na Kusafirisha Wageni na Watalii  kwenda Visiwani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji hichio Bwana Mataka Makame amemuomba Balozi Seif kwa kuitaka Serikali Kuu kufikiria kuwapatia Vyombo vya Uvuvi pamoja na Vifaa vyake ili kuendeleza kazi zao Bahari Kuu kwa vile eneo la sasa limekuwa na upungufu wa Samaki.

Balozi Seif pia alikaguwa Maendeleo ya Ujenzi wa Skuli ya Maandalizi ya Bweleo, Ujenzi wa Kiwanja cha Kisasa cha Michezo chenye hadhi ya Kimataifa , kuangalisha shughuli za Ushirika wa Akina mama wa Ukweli ni Njia Safi pamoja na Mradi wa Ufugaji Lulu ulio chini ya UItaalamu wa Taasisi ya Sayansi ya  Chuo Kikuu cha Dar es salaam iliyopo Forodhani.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

MAAJABU: JAMAA ANATEMBEA JUU YA MAJI

TAHADHARI: TANZANIA YAKUMBWA NA UGONJWA USIO NA TIBA WALA CHANJO

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), tarehe 20 Oktoba, 2012 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda.

Maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kabale, Kanda ya Kusini Magharibi ya nchi, na wilaya hii inapakana na Rwanda. Mpaka tarehe 24 Oktoba 2012, takriban watu 13 wamepata maambukizo na 6 wamepoteza maisha..

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale waliopo katika mikoa ambayo inapakana na na nchi jirani ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera na Kigoma).

Marburg ni ugonjwa wa hatari unaofanana na Ebola na unasababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalam “Marburg Virus”.

Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinazosababisha kutokwa damu mwilini, (Viral Haemorrhagic Fevers).

 Chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa huu haki­julikani. Hali inayosababisha mlipuko wake pia haijulikani. Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo.

Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na Homa kali, inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili yaani pua, njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, masikioni, machoni, hali inayopelekea kifo kwa muda mfupi.

 Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 3 hadi 9 baada ya kupata maambukizi.

Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na ha­raka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine iwapo mtu atakuwa karibu na mgonjwa na kugusana na mate, damu, mkojo, machozi, kamasi, maji maji mengine ya mwili, ikiwa ni pamoja na jasho au kumgusa  mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Marburg.

Ugonjwa huu pia unaweza kuenezwa iwapo mtu atagusa nguo au mashuka ya mgonjwa wa Marburg.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:

    Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya. Aidha taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),  “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli na vipeperushi vinavyoelezea ugonjwa huu.

    Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipaka. Aidha watalaamu hawa wa Afya pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.

    Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya


Taarifa  hii imetolewa na Kitengo cha mawasiliano ya Serikali

TAARIFA ZA MICHEZO KUTOKA TFF

PONGEZI KWA UONGOZI MPYA SIMIYU FA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Simiyu (SIFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba 27 mwaka huu).

Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SIFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Simiyu.

TFF inaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamati ya Utendaji ya SIFA ambayo ndiyo ya kwanza kuchaguliwa katika mkoa huo mpya chini ya uenyekiti wa Epafra Swai.

Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu Simiyu kwa kuzingatia katiba ya SIFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.

Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SIFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.

Viongozi waliochaguliwa ni Epafra Swai (Mwenyekiti), Kahema Manyili (Makamu Mwenyekiti), Sosie Chalamila (Katibu Msaidizi), Shabani Mwiko Aziz (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF) na Thomson Mtani (Mwakilishi wa Klabu TFF).

AY KUMTAMBULISHA MSANII ATAKAYEKUWA CHINI YAKE JUMAPILI HII

Friday, October 26, 2012

Rapper/muimbaji na hitmaker wa Party Zone, Ambwene Yesaya aka AY amesema Jumapili hii kwenye ukumbi wa Billcanas atamtambulisha rasmi msanii wa kike ambaye atakuwa chini ya kampuni yake ya Unity Entertainment.

Akiongea na XXL ya Clouds FM leo, AY amesema pamoja na msanii huyo wa kike, atakuwa na msanii mwingine wa kiume ambaye atamtaja siku za usoni.

Ameongeza kuwa kampuni yake imewekeza hela nyingi kwa wasanii hao kwaajili ya kufanya video na audio za kimataifa kwakuwa kwa sasa anafanya kazi kiprofesheno zaidi.

Ili kuwatangaza, AY amesema atakuwa akitembea na wasanii hao kwenye show zake atakazokuwa akifanya sehemu mbalimbali.

Jumapili hii yeye na Cpwaa watakuwa na show waliyoipa jina la Road2CHOMVA2012 kwaajili ya kujiandaa na tuzo za Channel O za mwaka huu ambapo wote wanawania vipengele kadhaa. (Bongo5.com)

HABARI LEO: MUAMSHO INATUMIWA NA WAHUNI - TUME

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesema wakati kuna madai kwamba Jumuiya ya Uamsho ni ya kidini (Kiislamu), lakini imekuwa ikitumiwa na makundi ya wahuni ambayo yamejipachika majina tofauti.

Taarifa ya Tume hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana ikiwa imesainiwa na Kamishna wake, Zahor Khamis, imetaja baadhi ya majina ya makundi hayo kuwa ni Mbwa mwitu, Simba mkali, Ubaya ubaya na Toto tundu na kuongeza kuwa yamekuwa yakitumika kufanikisha azma yao.

Mbali na jumuiya hiyo kutumiwa na wahuni, Tume pia imesema kutekwa kwa kiongozi wa jumuiya hiyo, Shekhe Farid Hadi Ahmed, kuna utata mkubwa ambao unahitaji uchunguzi na ufafanuzi kufahamu huko alikotekwa na kutoa mfano wa madai ya kunyimwa kula kwa siku tatu bila kuathirika kiafya.

Tume hiyo imehoji kama kweli alikuwa ametekwa, aliwezaje kufika msalani ambako alikuwa akinywa maji, wakati alikuwa amefungwa kitambaa usoni na mikononi akiwa na pingu na ilikuwa nyumba ambayo haijui! Kutokana na utata huo, Tume imemtaka Shekhe Farid kutoa maelezo yanayothibitisha pasipo shaka ili kuwathibitishia Wazanzibari, Watanzania na ulimwengu kwa jumla, juu ya kutoweka kwake.

“Shekhe Farid amedai alitekwa na watu wasiojulikana tarehe 16 mwezi huu na kuonekana siku tatu baadaye akiwa katika hali ya uzima na salama jambo ambalo lilisababisha vurugu kubwa Zanzibar na kusimama kwa shughuli zote za kiuchumi na kijamii,” ilieleza taarifa hiyo ya Tume.

Kwa mujibu wa Tume, kutokana na fujo hizo zilizotokea, hasara ilitokea ambayo mpaka sasa haijajulikana thamani askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Said Abdulrahman kuliuawa.

Kutokana na matukio hayo, Tume imeishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuwatafuta na kuwakamata wote walioshiriki katika vurugu hizo na kuvunja vikundi vyote vya kihalifu vilivyoanza kushamiri Zanzibar.

“Tunalaani mauaji ya askari Abdulrahman kwani ni uvunjaji wa haki za biaadamu, inapingana na sheria za nchi na ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 14 inayozungumzia haki ya kuishi na Katiba ya Zanzibar ibara ya 13 inayozungumzia haki ya kuwa hai,” taarifa hiyo ilifafanua.

Tume pia imelaani kitendo alichofanyiwa Diwani wa CCM Wadi ya Chumbuni kwa kushambuliwa na kujeruhiwa, kitendo ambacho kinakwenda kinyume na haki za binaadamu na Katiba ya Tanzania inayopiga marufuku mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au adhabu za kumdhalilisha.

“Kuna uhusiano gani wa kutekwa kwa kiongozi wa Uamsho na hujuma za mali za watu na CCM?” Taarifa hiyo ilihoji. Kwa mujibu wa Kamishina wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa Polisi inafanya uchunguzi wa kina kubaini kama Shekhe Farid anahusika na mtandao hatari wa ugaidi wa Al-Qaeda.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Mussa alisema Polisi nchini inafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa ikiwamo Polisi - Interpol.

“Jeshi la Polisi nchini kwa sasa linafuatilia kwa karibu sana nyendo zote za kiongozi wa Uamsho Shekhe Farid ikiwamo kuhusishwa kwake na mtandao wa Al-Qaeda,” alisema.

ZIARA YA BALOZI WA CHINA KWA VYOMBO VYA HABARI NCHINI

Na Ramadhan Ally-Maelezo Zanzibar    25/10/2012

China imeahidi kuendeleza azma yake ya kusaidia sekta za habari nchini kwa kuwapatia Mafunzo wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar bibi Chen Qi Man ameeleza hayo alipofanya ziara ya kutembelea vyombo vya habari vya Serikali ikiwemo Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC),Shirika la Magazeti na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Bi Chen amesema mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu yataongezwa kwa wafanyakazi wa vyombo hivyo katika fani za uandishi wa habari,ufundi na utawala ili kuimarisha utendaji kazi wa vyombo hivyo.

Amezitaka taasisi hizo za habari kuandaa wafanyakazi wanaostahiki kupata mafunzo hayo hapo mwakani kwa mujibu wa fani zao.

Akizungumzia suala la Mtambo wa kuchapishia magazeti ya Shirika la Magazeti la Zanzíbar,Bi Chen amesema amewasilisha ombi hilo kwa Serikali yake ambapo kwa sasa wanasubiri jawabu kutoka Serikali ya China.

Mapema Mhariri Mtendaji wa Shirika hilo Abdulla Mohammed amemuelezea Balozi huyo mdogo kuwa wana mpango wa kuanzisha Gazeti la Kingereza lakini wanashindwa kutokana na gharama kubwa za uchapaji unaofanyika huko Dar es Salaam ambapo mtambo huo haupo Zanzibar.

Kwa upande wake Waziri wa Habari,Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya China kwa misaada mbalimbali inayotoa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Sekta mbalimbali ikiwemo ya Habari.

Amemuelezea Balozi huyo kwamba kwa sasa Shirika la Utangazaji Zanzibar limo katika kipindi cha mpito kutoka Mfumo wa Analojia kwenda Dijitali kuanzia mwezi Januari hivyo watendaji wa Shirika hilo wanahitaji mafunzo zaidi katika mfumo huo mpya.

Aidha amemuelezea Balozi huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaandaa Sherehe kubwa za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zinatarajiwa kuhusisha mashindano ya mpira wa miguu kutoka timu mbalimbali za Taifa hivyo amemuomba Balozi huyo kuanza maandalizi ya kuiarifu timu ya Taifa ya China kushiriki mashindano hayo mwaka 2014

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Wednesday, October 24, 2012

SMZ YAVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUCHUNGUZA KWA KINA SAKATA LA KUTOWEKA KWA SHEIKH FARID NA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA WIKI ILIYOPITA

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMEVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA  NCHINI KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA ILI  KUBAINI  KIINI  CHA KUTOWEKA   SHEIKH FARID HADI  AHMED NA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA NCHINI WIKI ILIYOPITA..

KWA MUJIBU WA TAARIFA  ILIOTOLEWA NA WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS  ZANZIBAR MH. MOHAMMED ABOUD AMESEMA

KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA  KWA SHEIKH FARID KULIPELEKEA KUZUKA KWA MACHAFUKO KATIKA MAENEO KADHAA YA MJI WA ZANZIBAR AMBAPO MALI ZA WATU ZILIPORWA NA KUHARIBU MIUNDO MBINU YA BARABARA NA KUCHOMA MOTO MASKANI ZA CCM..

HIVYO ILITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUFANYA TATHMINI ILI KUJUA KIWANGO CHA HASARA KILICHOTOKANA NA VURUGU HIZO NA  KUWACHUKULIA HATUA  ZA KISHERIAWALE WOTE WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA KADHIA NZIMA YA SHEIKH FARID,VURUGU NA MAUAJI YA ASKARI KOPLO SAID ABRAHMANI HUKO  BUBUBU WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.

AIDHA VYOMBO HIVYO VIMETAKIWA KUENDELEA NAKUDHIBITI  HALI YA USALAMA WA NCHI KWA WAKATI WOTE KWA VILE VITENDO HIVYO

VIMEKUWA VIKIJITOKEZA MARA KWA MARA NA KUHAKIKISHA KWAMBA HAVIREJEI TENA.

TAARIFA HIYO ILIENDELEA KUSISITIZA WANANCHI KUACHA VITENDO VYENYE KUHATARISHA AMANI NA UTULIVU ULIOPO NCHINI KWA VILE CHUKI NA FUJO SIKU ZOTE KAZI YAKE NI KUBOMOA NA SIO KUJENGA.

MH. ABOUD ALIENDELEA KUSEMA KUWA  WALE WOTE WENYE DHAMIRA YA KUGOMBANISHA  WANANACHI NA SERIKALI YAO  NI VYEMA WAACHE KUFANYA HIVYO BALI JAMBO LA MSINGI  NI KUDUMISHA MASHIRIKIANO  ILI KUJENGA NCHI YETU KWA MASLAHI YA TAIFA NA VIZAZI VIJAVYO.

AMESEMA KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAWASHUKURU WANANCHI WOTE KWA USTAHAMILIVU WAO NA PIA KUVISHUKURU VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KWA KAZI NZURI WALIOIFANYA  KUTULIZA FUJO NA VURUGU AMBAPO HIVI SASA HALI IMEREJEA KUWA  YA UTULIVU.

 ALIONGEZA KUWA HIVI SASA  VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VINAENDELEA KUDHIBITI HALI HIYO NA KUWAOMBA WANANCHI WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZA KAWAIDA BILA YA WASIWASI.

KUHUSU UCHUMI WANCHI, ALISEMA KUWA ADUI MKUBWA WA UCHUMI  NI KWA NCHI KUINGIA KATIKA VURUGU NA MACHAFUKO KUNAKOPELEKEA KUVUNJIKA KWA AMANI NA UTULIVU  AMBAPO ZANZIBAR UCHUMI WAKE MKUBWA NI KUTOKANA NA SEKATA MAMA YA UTALII AMBAO HUATHIRIKA SANA KUKIKWA HAKUNA AMANI NA UTULIVU NA KUREJESHA NYUMA MAENDELEO NA KUZIDISHA HALI YA UMASIKINI JAMBO AMBALO HUONGEZA UPUNGUFU WA AJIRA KWA VIJANA WETU

WAZIRI HUYO  AMEWASIHI WANANCHI WA ZANZIBAR HASA VIJANA KULINDA AMANI YA NCHI AMBAYO NDIO RASILMALI KUU YA TAIFA.

ALISEMA KUWA PANAPOTOKEA TATIZO AU CHANGAMOTO YA AINA YOYOTE KWA MUJIBU WA MISINGI YA UTAWALA BORA NA WAKIDEMOKRASIA  NI BUSARA KUFANYIKA KWA MAZUNGUMZO MIOUNGONI MWA WADAU WAHUSIKA.

TAARIFA HIYO IMEONGEZA KUWA  WAZANZIBARI WOTE NI NDUGU, NI WATU WAMOJA  HAKUNA BUDI KUPENDANA, KUAMINIANA, NA KUSAIDIANA KWA HIVYO VIACHWE VITENDO VYENYE KUHATARISHA AMANI NA UTULIVU ULIOPO CHUKI NA FUJO HAZIANNAFASI KATIA ULIMWENGU HUU, KWANI VITU HIVYO KAZI YAKE NI KUBOMOA  NA SI KUJENGA

I SHEIKH FARID NA WENZAKE WANATARAJIWA KUFIKISHWA TENAKATIKA MAHKAMA YA MWANAKWEREKWE  HAPO KESHO .

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR. 24/10/2012

USHAURI WA RAMA DEE KWA LORD EYES KUHUSU KASHA YA WIZI WA VIFAA VYA GALI LA OMMY DIMPLES

Baada ya Loard Eyez kutuhumiwa Kumuibia Ommy Dimpoz vifaa vya gari lake, wasanii na wadau mbali mbali walitoa maoni yao kuhusu tuhuma hizi...lakini hivi karibuni kupitia ukurasa wa facebook, mkali wa R&B ambae yuko nchini Australia ametoa maoni yake kuhusu tukio hili ikiwa ni pamoja na kumshauri Mweusi Lord Eyez toka Arusha, Rama Dee ameandika stautus hii;

"loyd eyez naomba ubadilike kama ukishindwa kubadilika hapa basi,hakuna natakaye weza kukubadilisha hii imefikia sehemu mbaya na aibu hata kuiongelea,badilika ishi kama upo juu ya mika 20,uwe umeiba au haujaiba kutokana na utumiaji wako wa madawa ya kulevya lazima utahusishwa...saidia familia yako kwa kipaji ulicho barikiwa kweli inanisikitisha sana,mimi naomba niondolewe kwenye unafki wa kutetea ujinga,mchizi hali yake mbaya sio nzuri gari limewaka anahitaji msaada Alafu wewe dogo ommy kama ushahidi ikijulikana mchizi hajahusika juwa show zako zitaishia Chalinze ila pale Arusha baadae sana...".

VIJANA WENGI WAJITOKEZA KUJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA URAIA WILAYA YA KUSINI UNGUJA

Na Mohammed Mhina, Zanzibar

Zaiidi ya aslimia 80 ya wakazi wa wilaya ya Kusini Unguja Zanzibar wamejitokeza kujiandikisha kupata vitambulisho vya Taifa wengi wao wakiwa ni vijana.

Mkurugenzi wa Vitambulivyo vya Taifa Zanzibar Bw. Vuai Mussa Suleiman, amesema kuwa zoezi hilo lililoanza mwanzoni mwa mwezi huu  limeonyesha mafanikio na Jumatatu ijayo ya Oktoba 29, 2012 zoezi hilo litaingia katika wilaya ya Kati katika mkoa huo wa Kusini Unguja.

Bw. Vuai alikuwa akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari aliofuatananao katika ziara ya pamoja ya kuvitembelea vituo hivyo vya kujiandikishia katika wilaya ya Kusini unguja zoezi ambalo lilianza Oktoba 15, mwaka huu na linatarajiwa kumalizika kesho Alhamisi Oktoba 26, 2012.

Bw. Vuai amewataka wananchi wa wilaya zingine kujiandaa kwa kupiga kopi baadhi ya vielelezo muhimu vikiwemo vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa ili kurahisisha utekelezaji wa zoezi hilo.

Wakati wa ziara hiyo baadhi ya wasimamizi na masheha waliopo katika vituo hivyo wameelezea mafanikio na changamoto zinazojitokeza ambapo wamesema baadhi ya watu wanaofika kujiandikisha hawaelewi hata maana na foto kopi.

Msimamizi wa Kituo cha Bwejuu Bw. Khamisi Mabrouk Mbaraka,baadhi ya watu wanaofika katika vituo vyao wanapeleka hati halisi pasipo na kopi.

Nao baadhi ya Mashehe wamesema kuwa hakuna uwezekano wa mtu asiyehusika kujipenyeza na kujiandikisha kwa sababu watu wote wakiwemo wasio na vitambulisho vya Uzanzibar Mkazi wanaoshi katika shehia zao wameorodheshwa majina na kwamba ikijitokeza utata Sheha anawajibika kulitatua kwa kupitia kumbukumbu za wakazi wa eneo lake.

Akizungumza katika kituo cha Bwejuu, mmoja ya watu waliofika kujiandikisha Bi. Mwakito Mkadamu, ameelezea umuhimu wa vitambulisho hivyo kwa jinsi alivyoelimishwa kupitia vyombo vya habari na kusema kuwa kinaweza kumsaidia katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na kiuchumi.

Miongoni mwa watui wanaojiandikisha kupata vitambulisho hivyo wapo wa kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara wanaoishi Zanzibar kwa shughuli binafsi na za kikazi.

JESHI LA POLISI ZANZIBAR KUFUNGA BAADHI YA BARABARA SIKUU YA EDDI EL HAJI

Na Mwanshi wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Jeshi la Polisi zanzibar limetangaza kuzifunga baadhi ya barabara za mji wa Zanzibar ili kuwawezesha wananchi wakiwemo watoto wadogo kusherehekea siku kuu ya Eddi el Haji kwa usalama na amani.

Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amezitaja baadhi ya barabara zitakazofungwa kwa muda wa siku nne kuanzia Ijumaa wiki hii hadi Jumatatu wiki ijayo kuwa ni ile inayotoka Mnazi Mmoja hadi Viwanja vya michezo vya Maisala, barabara ya kutoka Ofisi ya Baraza la Wawakilishi la Zamani kuelekea Viwanja vya Maisala na Barabara ya ya kutoka Ukumbi wa CCM kuelekea Mnazi Mmoja.

inspekta Mhina, amesma kuwa barabar hizo zitafungwa kuanzia majira ya saa 9.00 arasili hadi saa 4.30 usiku kwa kila siku muda ambao watu wengi watakuwa wamesharejea majumbani kwao baada ya kusherehekea siku hiyo.

Awali akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Zanzibar, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Ungauja ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa sherehe hizo zitaadhimishwa kwa muda wa siku nne mfululizo zitaanza Ijumaa ya Oktoba 26 hadi Jumatatu ya Oktoba 29 2012.

Katika hatua nyingine Kamanda Aziiz amesema Jeshi la Polisi mkoani humo litaweka vituo vidogo vya Polisi katika maeneo yote ya viwanja vikubwa vitakavyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu kwa lengo la kuwahakikishia wananchi ulinzi wa usalama wao pamoja na mali kwa wakati wote wa sherehe hiyo.

Kamanda huyuo amevitaja viwanja vitakavyokuwa na mikusanyiko mikubwa kwa ajili ya sherehe hizo za Eddi El Haji  kuwa ni Mnazi Mmoja, uwanja wa Demoklasia, Jamhuri Garden, Forodhan Park, Kiembe Samaki, Nyarugusu, Maungani na Bububu Meli nne.

Kamanda Aziz amesema Kiwanja cha michezo cha Kariakoo mjini Zanzibar kwa mara nyingi hakitaweza kutumika kutokana na kuharibika.

Amewataka waqzazi na walezi kutowapa vijana wao makundi makubwa ya watoto wadogo ili kuepuka kupoteana katika viwanja hivyo ambavyo mara nyingi vinakuwa na umati mkubwa wa watu.

Amewakumbusha wazazi na walezi hao pia kutowaruhusu watoto wao kwenda karika fukwe za bahari kuogelea pasipo uwangalizi wa watu wazima kwani amesema kuwa uzoefu unaonyesha kuwa watoto huzama na kufa maji baharini pasipokuwa na uwangalizi katika nyakati za siku kuu kama hizi.

Hata hivyo Kamanda Aziz amewataka wazazi kuwaelimisha watoto wao kuwa wanapobaini kupotezana na ndugu na jamaa zao wafike katika vituo hivyo vidogo vya Polisi na yeyote atakayepotelewa aweze kufika hapo kwa utambuzi na kumpata mtoto wake.

Amewakumbusha wananchi kutoziacha nyumba na sehemu zao za biashara pasipo na uwangalizi wa kutosha wanapotoka kwenda katika viwanja vya burudani ili kuepuka kuwapa wezi fursa ya kupora mali zao.

Kwa upande wa madereva kamanda aziz amewataka madereva wote kuendesha vyombo vyao kwa mwendo wa kadri na kuepuka kuvunja sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani na kwamba kwa yeyote atakayekaigi agizo hilo hatua kazi zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Visiwani Zanzibar sherehe za Eddi El Fitri na Iddi El haji ndizo sherehe kuwa kupita zote za kiserikali na husherehekewa kwa muda wa siku nne mfululizo katika viwanja mbalimbali ingawa utaratibu huo wa kusherehekea hauingiliani na na ule uliopo kwenye kalenda ya Serikali.

UNION OF TANZANIANS IN GERMANY (UTU) KUKUTANA NA WAFADHILI NA WAHISANI ZAIDI YA 150 !!!! WORLD MISSION SUNDAY 28.OCT. 2012

Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)  Unapenda kuwakaribisha Watanzania wote wanaoishi ujerumani, Katika Hafla ya WORLD MISSION SUNDAY. itakayofanyika Katika ukumbi Uliopo Hauptstr. 30, D-63814 Mainaschaff Jirani sana na Mji wa Aschaffenburg Siku ya Jumapili Tarehe 28.10.2012, Kuanzia saa 04:00  za Asubuhi.

Ambapo Wasamaria wema na Wafadhili wapatao zaidi ya 150 kutoka sehemu mbali mbali za ujerumani watakutana na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) Juu ya kuitakia mema Tanzania na kuanzisha Harambee ya kuchangia maendeleo ya miradi mbali mbali itakayosimamiwa na Umoja wa watanzania Ujerumani (UTU).

Katika Hafla hiyo Kuanzia saa  9 mchana watayarishaji wa Hafla hiyo ''World Mission Sunday'' itatoa nafasi kwa Umoja wa Watanzania Ujermani (UTU) Kuitambulisha Tanzania Kwa wahisani hao , na kuelezea ni mradi gani unahitaji  ufadhili kupitia Umoja huu.  Mmoja wa wageni rasmi walio alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Ahmada Ngemera, Dr. Lippert na mkewe Kutoka Scheinfurt' Dr. Lippert ni mtaalamu ambaye aliwahi kufanya kazi Tanzania.

Hafla hii inategemewa kuisha saa 12:00 za jioni, baada ya hapo watanzania watapata muda wao wa kufanya mazungumzo na Mhe: Balozi wa Tanzania Nchini ujerumani Bw. Ahmada Ngemera.

Umoja wa Watanzania Ujerumani  UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee  Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.

Tunawaomba Watanzania Wote  na marafiki wa Tanzania  wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Karibuni sana ! Umoja Ni Nguvu

DR. SHEIN AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI NA WATENDAJI SMZ

Tuesday, October 16, 2012

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilieleza kuwa, Dkt. Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 43 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 amemteua Mhe. Shawana Bukheti Hassan kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. Uteuzi huo umeanza jana 15 Oktoba 2012.  

Aidha, kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu 48(a) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amefuta rasmi uteuzi wa Mheshimiwa Mansoor Yussuf Himid kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. 

Mheshimiwa Rais amemuondosha Mheshimiwa Mansoor Yusuf Himid katika madaraka ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi kuanzia jana tarehe 15 Oktoba 2012.  

Dkt. Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 47 cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 amefanya uteuzi wa Naibu Mawaziri ambapo Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak ambapo pia, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  anakuwa Mhe. Mohammed Said Mohamed.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 50 (2) na 50 (3) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano 
Dkt. Juma Malik Akili. Aleikuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Vuai Iddi Lila atapangiwa kazi nyengine.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati  Bw. Ali Khalil Mirza. Aliekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Mwalim Ali Mwalim atapangiwa kazi nyengine.  
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 50 (4) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara kama ifuatavyo:
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano 
Bw. Tahir M. Abdulla. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Msanif Haji Mussa atapangiwa kazi nyengine.
 
Aidha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati 
Bw. Mustafa Aboud Jumbe ambaye anachukua nafasi ilioachwa wazi na Bw. Tahir M. Abdulla aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.
 
Pia, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anaeshughulikia Idara Maalum za SMZ 
CDR  Julius Nalimy Maziku ambaye anajaza nafasi ilioachwa wazi na Capt. Juma Abdulla Juma alieteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari hivi karibuni.
 
Pamoja na hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo)- Bw. Juma Ameir Hafidh ambaye anachukua nafasi ilioachwa wazi na Bw. Abdi Khamis Faki alieteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato (ZRB) hivi karibuni.
 
Dkt. Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 11 cha Sheria ya Utalii Namba 6 ya 2009 kama kilivyorekebishwa na Kifungu 12 cha Sheria ya Utalii (Marekebisho) Namba 7 ya 2012 amemteua Bw. Saleh Ramadhan Ferouz kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii ambaye anachukua nafasi ilioachwa wazi na Bw. Ali Khalil Mirza alieteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Namba 1 ya 2012 amemteua Bw. Mussa Haji Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi.  
Uteuzi huo umeanza jana tarehe 15 Oktoba 2012.

UNION OF TANZANIANS IN GERMANY (UTU) KUKUTANA NA WAFADHILI NA WAHISANI ZAIDI YA 150 !!!! WORLD MISSION SUNDAY 28.OCT. 2012

Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)  Unapenda kuwakaribisha Watanzania wote wanaoishi ujerumani, Katika Hafla ya WORLD MISSION SUNDAY. itakayofanyika Katika ukumbi Uliopo Hauptstr. 30, D-63814 Mainaschaff Jirani sana na Mji wa Aschaffenburg Siku ya Jumapili Tarehe 28.10.2012, Kuanzia saa 04:00  za Asubuhi.

Ambapo Wasamaria wema na Wafadhili wapatao zaidi ya 150 kutoka sehemu mbali mbali za ujerumani watakutana na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) Juu ya kuitakia mema Tanzania na kuanzisha Harambee ya kuchangia maendeleo ya miradi mbali mbali itakayosimamiwa na Umoja wa watanzania Ujerumani (UTU).

Katika Hafla hiyo Kuanzia saa  9 mchana watayarishaji wa Hafla hiyo ''World Mission Sunday'' itatoa nafasi kwa Umoja wa Watanzania Ujermani (UTU) Kuitambulisha Tanzania Kwa wahisani hao , na kuelezea ni mradi gani unahitaji  ufadhili kupitia Umoja huu.  Mmoja wa wageni rasmi walio alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe.

Ahmada Ngemera, Dr. Lippert na mkewe Kutoka Scheinfurt' Dr. Lippert ni mtaalamu ambaye aliwahi kufanya kazi Tanzania. Hafla hii inategemewa kuisha saa 12:00 za jioni, baada ya hapo watanzania watapata muda wao wa kufanya mazungumzo na Mhe: Balozi wa Tanzania Nchini ujerumani Bw. Ahmada Ngemera.

Umoja wa Watanzania Ujerumani  UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee  Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.

Tunawaomba Watanzania Wote  na marafiki wa Tanzania  wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Karibuni sana ! Umoja Ni Nguvu

SMZ YAOMBWA KUFIKIRIA MUUNDO WA MIRADI MBADALA YA KIUCHUMI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WAVUVI GHUBA YA CHWAKA

Saturday, October 13, 2012

Na: Othman Khamis Ame

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeombwa kufikiria muundo wa  Miradi mbadala ya Kiuchumi itakayosaidia kutoa ajira, kulinda Mazingira ya Bahari pamoja  na kupunguza msongamano wa wavuvi katika Ghuba ya Chwaka na Marumbi.

Muundo huo wa miradi Mbadala kwa njia nyengine pia utakuwa suluhisho la    kudumu la mgogoro wa muda mrefu wa uvuvi unaokaribia miaka 35 sasa kati ya Vijiji jirani vya Chwaka na Marumbi viliopo Wilaya ya Kati.

Ombi hilo limetolewa na Wananchi wa Kijiji cha Chwaka wakati wakitoa kero pamoja  na changamoto zinazowakabili mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika uwanja wa soka wa Chwaka Wilaya ya Kati.

Mkutano huo wa Balozi Seif ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa wakati alipokutana na Wananchi wa Marumbi kupokea kero na Matatizo yao miezi michache iliyopita ambayo yanavihusu Vijiji hivyo kwa pamoja kubwa hasa ni suala la Uvuvi.

Bwana  Vuaa Mwadini Mcha alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba idadi kubwa ya Wavuvi wanaofanya shughuli zao za Uvuvi katika ghuba ya Chwaka imekuwa kubwa kulinganisha na uwezo wa ghuba yenyewe.

Hata hivyo Bwana Vuaa alisema Wananchi wa Chwaka wako tayari wakati wowote kumeguka kwa asilimia kubwa kutoka katika shughuli za Uvuvi kama Serikali itaanzisha miradi ya Kiuchumi itakayowawezesha Wananchi hao kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku.

“ Tunakumbukumbu nzuri tusiyoisahau ya Rais wa Awamu ya Pili Mzee Aboud Jumbe Mwinyi wakati ule alipotutaka tuachane na uvuvi wa juwa. Kwanza alituwezesha kwa kutuletea nyavu na baadaye taaluma ya matumizi bora ya Bahari mpango ambao ulifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana”. Alifafanua Bwana Vuaa Mwadini.

Alimuhakikishia Balozi Seif kwamba Wananchi na Wavuvi wa Chwaka hawana ugomvi na Wananchi wa Marumbi lakini kinachojitokeza  ni Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Polisi Wilaya ya Kati kuwa na kigugumizi cha kuchukuwa hatua za kisheria  wakati yanapotokea matatizo hasa ya Uvuvi baina ya pande hizo mbili.

“ Chwaka haiko tayari Mwananchi ye yote  afariki kutokana na ugomvi wa Uvuvi. Lakini tumefikia wakati kukosa  imani dhidi ya  uongozi wa  Polisi na Serikali wa Wilaya ya Kati kwa kushindwa kuchukuwa hatua za kisherika kwa watu  wanaokiuka sheria hizo.

Naye Bwana Nuru Muhammad alielezea masikitiko yao kutokana na Mradi mkubwa ulioanzishwa chini ya uhadhili wa Benki ya Dunia wa kuwawezesha wavuvi wa Ghuba hiyo { Macemp } kutowanufaisha Wavuvi hao ambao ndio walengwa wa mradi huo.

Bwana Nuru alifahamisha kwamba  licha ya juhudi zilizochukuliwa na Wawakilishi wa Mradi huo kupitia wasimamizi wa Benki ya dunia wa kukutana na Wananchi hao kwa kupanga malengo ya mradi huo kiutekelezaji kwa vile mfuko wa mradi huo haukuwa na mashaka lakini kilichojichomoza zaidi kwa mfuko huo ni kuendelezwa kwa semina na vikao.

“ Inasikitisha kuona Vikao mbali mbali vilifanywa kwa kushirikishwa wavuvi husika lakini nguvu za mradi huo zikaelekezwa sehemu nyengine bila ya kuwanufaisha walengwa ambao ni sisi Wavuvi”. Alisisitiza Bwana Nuru.

Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alisema wajibu wa Serikali wakati wote ni kufuatilia na kujua kero zinazowakabili Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi unaostahiki. Balozi Seif alielezea kusikitishwa kwake na mgogoro wa uvuvi  unaotia doa mfumo wa amani na utulivu Nchini unaovikumba Vijiji vya Chwaka na Marumbi kwa karibu miaka 35 sasa.

“ Sisi tunataka amani na utulivu, watu waishi pamoja, wafanye kazi pamoja, haya mambo ya Ukafu  na uccm hayana nafasi tena katika Jamii. Tunachokizingatia zaidi kwetu sisi kama Serikali ni kuona wananachi wanaishi kwaamani na  kushirikiana pamoja”. Alisisitiza Balozi Seif.

Katika Mkutano huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliahidi kutoa Mabomba 800  pungufu yaliyooelezwa ndani ya risala ya Wananchi hao wa Chwaka  kukamilisha Mabomba 1200 yaliyokisiwa kutumika katika mradi wa Maji safi na Salama katika Shehia hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi,  Makazi, Maji na  Nishati Mh. Ramadhan Abdulla  Shaaban aliahidi kugharamia ujenzi wa Tangi la Maji ili kukamilisha mradi huo muhimu.

Hata hivyo  Waziri Shaaban aliwanasihi Wananchi hao wa Chwaka kuwa na stahamala  kidogo kwa vile kazi hiyo inahitaji gharama ambayo kwa hivi sasa  itahitajika kutafutiwa  bajeti yake.

Aliwataka Wananchi hao wa Chwaka kuwa tayari wakati utapowadia       kuitekeleza kazi hiyo  kwa ushirikiano na  Watendaji wa Taasisi za Wizara hiyo kwa njia ya mpango wa ujenzi wa Taifa.

KAMADA WA POLISI MKOANI MWANZA AUAWA NA WATU WASIOJULIKANA KWA KUPIGWA RISASI

Taarifa zilizopatikana kutoka jijini Mwanza zainasema usiku wa kuamkia leo majira ya saa  8 usiku   Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow ameuawa kwa kupigwa risasi usiku huu maeneo ya hotel Tai 5, Kitangili jijini Mwanza .
 
Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alifariki kabla ya kufikishwa katika hospitali ya Bugando ambapo inadaiwa alivamiwa na watu waliokuwa wamevalia mavazi ya polisi jamii ndipo aliposimamishwa na baada ya kusimama watu hao walimmiminia risasi kufuani na kupelekea kifo chake
 
Imeelezwa kwamba Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alikuwa akitoka kwenye harusi na alikuwa na mtu mmoja  kwenye gari aliyekuwa akimsindikiza mtu huyo ambaye ni mwanamke yeye hakudhurika na chochote katika tukio hilo.
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Eng. Evarist Ndikilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya uliNzi na usalama mkoani humo ameshathibitisha kutokea kwa tukio hilo la kifo cha kamanda Liberatus Barlow

UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA DAR ES SALAAM (DRFA)

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA DAR ES SALAAM (DRFA)
Oktoba 12, 2012
 
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekamilisha usikilizaji rufani zilizokatwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA.
 
Ili kujiridhisha kuhusu uamuzi wote uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA kuhusu waombaji uongozi wote wa DRFA waliopitishwa na ambao hawakupitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA, Kamati itatangaza uamuzi wake kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi wa DRFA siku ya Jumanne, Oktoba 16, 2012.
 
Kutokana na hali hiyo, Uchaguzi wa DRFA uliokuwa ufanyike Oktoba 14, 2012 umeahirishwa hadi hapo uamuzi kuhusu uchaguzi huo utakapotangazwa Jumanne, Oktoba 16, 2012.
 
Angetile Osiah
Katibu Mkuu
Katibu- Kamati ya Uchaguzi TFF

WAZIRI WA HABARI ZANZIBAR AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA

Thursday, October 11, 2012

Na YUSSUF SIMAI.MAELEZO ZANZIBAR.10/10/2012.

Wazi wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarou amesema kuwa Zanzibar itahakikisha inaingia katika Mfumo wa Digital kabla ya kufikia tarehe iliowekwa ili kwenda sambamba na mabadiliko ya Ulimwengu.

Waziri ameyasema hayo hapo Afisini kwake Kikwajuni wakati alipofanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diane Conrner .

Amesema licha ya Zanzibar kuingia katika Mfumo wa Digital lakini inakabiliwa na  changamoto nyingi ikiwa pamoja na Vifaa na mafunzo kwa watendaji wake.

Akizungumzia Sekta ya Utalii Waziri Mbarouk alisema kuwa sekta hio inakua kwa kasi kubwa  kutokana na Wawekezaji Binafsi ambao huwekeza Zanzibar na kuweza kuitangaza zaidi katika miji na Nchi tafauti.

Aidha maesema kuwa Serikali inafarijika kuona Watalii wengi kutoka Uingereza na nchi nyengine za Ulaya wanafika  Zanzibar na kutembelea sehemu mbalimbali za kihistiria na vivutio vyengine vya Utalii vilivyopo nchini.

Nae Balozi huyo Diane Conrner ameipongeza Zanzibar kwa juhudi kubwa inazochukua katika kuimarisha sekta ya utalii na kueleza matumaini yake kuwa sekta hiyo itaendelea kuwa muhimili mkubwa wa uchumi.

Akizungumzia sekta ya michezo Balozi Diane ameishauri  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar kushiriki michezo mbali mbali ikiwemo  ya Kimataifa kwa vile michezo  inatoa mchango mkubwa katika kuitanga nchi  kujulikana duniani kote.

Akitoa mfano wa Michezo ya Olimpiki iliofanyika mjini London, Uingereza, mwaka huu amesema  imeweza kuipatia sifa kubwa Nchi yake pamoja na Faida mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Waziri Saidi amemshukuru Balozi huyo kwa Kufika kwake Zanzibar na kuweza kuzungumza na viongozi masuala mbalimbali yenye umuhimu kwa nchi na jamii kwa jumla.

METOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

STANBOI ATOA BURE ALBUM YAKE "THOUGHTS OF AN AFRICAN CHILD" "

Monday, October 8, 2012

Wiki hii msanii wa Tanzania aishie nchini Marekani Stanboi aka The African Child ameachia albam yake iitwayo ‘Thoughts of An African Child’ bure mtandaoni.

“Its that time people............You can now download my debut EP "THOUGHTS OF AN AFRICAN CHILD" Vol 1 The EP for free download now on http://www.stanboimusic.com/albums/ I appreciate all the love and support that has come my way, without my fans I wouldnt be anything..............So I thank everyone from the depth of my heart..............DOWNLOAD, DOWNLOAD, DOWNLOAD.......Comment, Share, Repost, Lets spread it to ALL!!!,”

aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. (BONGO5)

NEW VIDEO: C-SIR MADINI - PAIN KILLER

Hii ni video mpya ya C-sir Madini ya wimbo wake mpya unaoitwa PAIN KILLER. Utaanza kuonekana kwenye TV stations siku si nyingi kutoka sasa, ila imekuwa released kwenye internet. Video imefanywa na Adam Juma na imefanyika Dar. Audio itafuata baada ya wiki moja.

IGP MWEMA ATAKA KILA MWANANCHI KUWA MLINZI WA TAIFA LETU

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amesema kuwa ili kuifanya nchi yetu iendelee kuwa salama, kuna haja ya kuwekeza zaidi katika miundombinu ya amani.

IGP Mwema ameyasama hayo leo mjini Zanzibar wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi wa kati kwa askari Polisi kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi mjini Zanzibar.

Amesema bado kuna haja ya kila mwananchi kuelewa kuwa jukumu la usalama wa nchi hii liko mikononi mwake.

Amesema kila mmoja hawezi kukwepa jukumu la kulinda rasilimali yake na mfano mdogo ni pale kila mmoja kwa wakati wake na bila ya kufundishwa pale anapolinda faragha.

IGP Mwema pia ameeleza umuhimu wa kwa nini kila Mtanzania anapaswa kuwa  mlinzi wa Taifa letu na kutilia mfano kwamba suala la ufalama linaanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, kaya, kijiji, kata ama shehiya tarafa wilaya mkoa na Taifa.

Amesema katika taaluma ya Polisi, Askari amefundishwa kuwa mlinzi katika mambo manne makubwa ambayo yanamhusi kila mmoja wetu bila ya kujali nafasi yake katika jamii.

Mambo hayo ni manne ni fursa ambazo zikiachwa wazi watu wengine wanachukua nafasi ya kuichukua nafasi kuu nne ( four Speces )  sio  kama askari lakini hatani  kabla ya wa mali wa mali zake, mlinzi wa familia wakiwemo watoto wake pamoja na himaya inayomzunguuka.

Amewataka Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake, awe mdau wa sualama kama anavyolinda na kuheshimu faragha zake.

Kwa upande wake, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuna haja ya kila kiongozi wa Jeshi la Polisi hapa nchini kuyageuza matazo wanayowakabili kama changamoto na kuzigeuza fursa ya kuleta ufanisi kazini.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mh. Abdallah Mwinyi, ameelezea mikakati inayochukuliwa na mkoa wake katika kudhibiti usalama wa maeneo mbalimbali na kusema kuwa Ulinzi shirikishi na Polisi Jamii ni jicho la Polisi mitaani.

Awali akitoa tathmini ya mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Zanzibat ACP Ramadhani Mungi, amesema wahitimu hao wamejifunza mambo mbalimbali ukiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Polisi na vyombo vya Habari.

Kamanda Mungi, amesema wameweka somo hilo kwa kufahamu kuwa kazi za Polisi zinaingiliana kwa kiasi kikubwa na zile za Waandishi wa Habari na kwamba kila mmoja anamtegemea mwingine ili kufanikisha kazi zake.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Kamishna Khalifa Hassan Choum, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Dar es Salaam ACP Ali Lugendo na Maafisa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Vikosi vya SMZ.Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

ZANZIBAR JUMAMOSI OKTOBA 6, 2012. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amesema kuwa ili kuifanya nchi yetu iendelee kuwa salama, kuna haja ya kuwekeza zaidi katika miundombinu ya amani.

IGP Mwema ameyasama hayo leo mjini Zanzibar wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi wa kati kwa askari Polisi kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi mjini Zanzibar.

Amesema bado kuna haja ya kila mwananchi kuelewa kuwa jukumu la usalama wa nchi hii liko mikononi mwake.

Amesema kila mmoja hawezi kukwepa jukumu la kulinda rasilimali yake na mfano mdogo ni pale kila mmoja kwa wakati wake na bila ya kufundishwa pale anapolinda faragha.

IGP Mwema pia ameeleza umuhimu wa kwa nini kila Mtanzania anapaswa kuwa  mlinzi wa Taifa letu na kutilia mfano kwamba suala la ufalama linaanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, kaya, kijiji, kata ama shehiya tarafa wilaya mkoa na Taifa.

Amesema katika taaluma ya Polisi, Askari amefundishwa kuwa mlinzi katika mambo manne makubwa ambayo yanamhusi kila mmoja wetu bila ya kujali nafasi yake katika jamii.

Mambo hayo ni manne ni fursa ambazo zikiachwa wazi watu wengine wanachukua nafasi ya kuichukua nafasi kuu nne ( four Speces )  sio  kama askari lakini hatani  kabla ya wa mali wa mali zake, mlinzi wa familia wakiwemo watoto wake pamoja na himaya inayomzunguuka.

Amewataka Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake, awe mdau wa sualama kama anavyolinda na kuheshimu faragha zake.

Kwa upande wake, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuna haja ya kila kiongozi wa Jeshi la Polisi hapa nchini kuyageuza matazo wanayowakabili kama changamoto na kuzigeuza fursa ya kuleta ufanisi kazini.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mh. Abdallah Mwinyi, ameelezea mikakati inayochukuliwa na mkoa wake katika kudhibiti usalama wa maeneo mbalimbali na kusema kuwa Ulinzi shirikishi na Polisi Jamii ni jicho la Polisi mitaani.

Awali akitoa tathmini ya mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Zanzibat ACP Ramadhani Mungi, amesema wahitimu hao wamejifunza mambo mbalimbali ukiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Polisi na vyombo vya Habari.

Kamanda Mungi, amesema wameweka somo hilo kwa kufahamu kuwa kazi za Polisi zinaingiliana kwa kiasi kikubwa na zile za Waandishi wa Habari na kwamba kila mmoja anamtegemea mwingine ili kufanikisha kazi zake.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Kamishna Khalifa Hassan Choum, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Dar es Salaam ACP Ali Lugendo na Maafisa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Vikosi vya SMZ.
Newer Posts Older Posts

UNAPOHITAJI kujua DUNIANI nini kimetokea, Basi fuatilia Kurasa Zangu za Kijamii TWITTER, FACEBOOK pamoja na INSTAGRAM, BONYEZA hapa >>> TWITTER, INSTAGRAM na FACEBOOK, PIA Unaweza Kujiunga na chaneli yangu ya YOUTUBE, ili kutazama Video >>>YOUTUBE

 

Copyright © 2010 NYUMBANI KWANZA. All Rights Reserved.