WANANACHI kisiwani Pemba, wamepongeza
hutuba ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali
Mohamed Shein, alioitoa kwenye kilele cha maadhimisho ya sherehe za elimu bila
ya malipo, yaliofanyika hivi karibuni kisiwani humo.
Walisema
hutuba hiyo ni miongoni mwa hutuba
kadhaa zinazotolewa na rais huyo na kuibua hisia, mawazo mapya ndani ya jamii,
jambo ambalo huwazidisha upendo kwa kiongozi wao.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, baadhi ya wananchi hao walisema,
hutuba hiyo ilikuwa imejaa kila aina ua tendaji, utekelezaji, ahadi na
mafanikio yaliopo ndani ya serikali anayoiongoza.
Mmoja katia
ya wazazi hayo, Abdull-hamid Juma Makame wa Mchanga mdogo wilaya ya Wete,
alisema yeye kwenye hutuba hiyo, lililomvutia ni pale rais alipotangaaza kufuta
michango ya elimu ya sekondari.
Alisema
tamko hilo kwake, limempa hisia mpya kwamba rais huyo amekuwa akiwajali
wanyonge wa nchi hii, kwa lengo la kuona watoto wote, wanapata elimu bila ya
kujali uwezo wa wazazi na walezi wao”,alifafanua.
Nae Mashavu
Himid Mbaruok wa Wingwi mapofu wilaya ya Micheweni, alisema mara zote rais huyo
wa Zanzibar anapotoa hutuba kwenye sherehe mbali mbali za kitaifa, hulenga kuwapatia
wananchi huduma sawa.
“Mimi
sikutarajia kuwa, kwa vile ameshafuta michango ya elimu ya msingi mwaka jana,
na atangaaze kufuta michango ya sekondari, lakini amefanifaya na mimi kama
mazazi mwenye watoto wanne mwakani wanaoingia sekondari napongeza”,alifafanua.
Hata hivyo Muhidini
Ameir Ali wa Machomane Chakechake,
alisema hutuba hiyo ya rais alioitoa Septemba 23, inafaa kuandikiwa kitabu
chake maalum, ili ihifadhiwe na ije isomwe na vizazi vijavyo.
Alisema
hutuba hiyo ya raisi, ilieleza historia ya kielimu Zanzibar kabla na baada ya
mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, ambayo skulini haisomeshwi.
“Mimi kwenye
hutuba hile ya rais, nililoliona kwangu ni kubwa na inafaa kuwekewa kumbu kumbu,
ni suala la historia ya elimu, na sasa ndani ya awamu hii ya saba
ilivyoimarishwa”,alieleza.
Kwa upande
wake Habiba Mjaka Kombo wa Mtambile, alisema kilichomvutia yeye kwenye hutuba
ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed
Shein, ni ahadi ya kujenga skuli tisa za ghorofa Unguja na Pemba.
Aidha
alisema jengine lililomvutia ni kuona jinsi rais alivyotekeleza upanuzi wa
skuli 23 na nyengine kufanyiwa matengenezo makubwa, ununuzi wa vifaa vya
maabara na samani.
Mwenyekiti
wa masheha wilaya ya Micheweni Dawa Juma Mashindo, alisema yeye alivutiwa na
kila jambo, ingawa rais kutangaaza kipaumbele cha kutanua elimu kilimkosha roho.
Septemba 23,
mwaka huu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: dk Ali
Mohamed Shein, alikamilisha kilelele cha maadhimisho ya siku ya elimu bila ya
malipo, uwanja wa Gombani kwa hutuba yake, alioeleza mambo kadhaa, ikiwa ni
pamoja na kutangaaza kufuta michago ya elimu ya sekondari.